HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2013

CHAMA CHA RIADHA TANZANIA YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO

Rais wa chama cha Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero akikabidhiwa mpango mkakati wa riadha kuelekea kwenye olympiki ijayo ya mwaka 2016 na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Utawala, William Kallaghe ambayo itafanyika Rio De Janeiro nchini Brazil katika hafla iliyofanyika mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati ya utendaji kituo cha michezo cha Highlands Kigurunyembe mkoani Morogoro. kulia ni Katibu wa Riadha Tanzania. Mujaya Nyambui na kushoto ni Mhazini wa chama hicho, Suleiman Ishigue.

MOROGORO, Tanzania


 SHIRIKISHO la riadha Tanzania limezindua mpango mkakati wa miaka mitano kuelezea mashindano ya Olympiki ambayo yatafanyika nchini Brazil Rep De Jenerio 2016.
Mpango huo ulikabidhiwa kwa Rais wa Riadha Tanzania, Anthony Mtaka, Mara baada kumalizika kwa kikao cha kamati ya utendaji cha chama hicho katika kituo cha Michezo cha the Highlands mjini Morogoro.

Akizungumzia mkakati huo, Rais wa chama hicho Mtaka akisema kuwa mpango huo una lengo la kuwezesha Tanzania kushiriki kikamilifu na kupata mafanikio makubwa ukilinganishwa na miaka iliyopita.

Katika mpango huu umeelezwa kuwa utawezesha Tanzania kushiriki kikamilifu katika mashindano mbalimbali ikiwemo ya All Africa Game hadi Olympic ya Rio De Janeiro nchini Brazil.
Kupitia mpango, programu mbalimbali za kuandaa wachezaji wenye umri tofauti kushiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

mbali na mpango huo mkakati pia kikao hicho kilipitia rasimu ya katiba mpya ya chama hicho.
Pia katika kikao hicho kilipitisha kufanyika kwa mashindano ya nyika ya taifa, Yatakayofnyika machi 10 mji Morogoro.

Mashindano hayo yatatumika pia kuchagua timu ya Taifa itakayoshiriki mashindano ya dunia machi 24 huko nchini Poland.
Kingine kilichopitishwa ni kalenda ya mwaka ya chama cha riadha Tanzania (RT) ambayo inatarajiwa kutumwa katika mikoa yote kwa ajili ya utekelezaji.

No comments:

Post a Comment

Pages