TORONTO,
Marekani
"Kila mmoja
anampa pole Torsten na hawataweza kumona akiiongoza Toronto msimu huu kutokana na kipindi kirefu
cha majeraha na hapo ndipo tatizo lilipo. Tunautambua na kuukubali mchango wa Torsten
kwa Toronto FC na
tueridhika maamuzi yake"
NYOTA wa zamani wa kimtaifa wa Ujerumani na nahodha wa klabu
ya Toronto FC, Torsten Frings, juzi Jumanne ametangaza kustaafu soka, akisema
hawezi kurejea dimbani akiwa fiti kutokana na upasuaji wa nyonga aliofanyiwa.
Frings, ambaye alishinda mechi 79 akiwa na timu ya taifa na
kucheza fainali mbili za Kombe la Dunia – ikiwamo waliyofika fainali mwaka 2002,
alitumia msimu mmoja na nusu akiwa na klabu ya Toronto ya Marekani.
Kutua kwake Marekani kulikuja baada ya kufanya mambo makubwa
katika Bundesliga alikozichezea klabu kongwe za Bayern Munich, Werder Bremen na Borussia Dortmund.
Frings, 36, kiungo-mkabaji mahiri, alikuwa mchezaji
anayelipwa pesa nyingi (milioni 2.43), lakini kipindi chake cha kuichezea Toronto ya Ligi Kuu ya
Marekani (MSL) kimekuwa kikikabiliwa na jinamizi la majeraha.
"Wakati huu tukiwa katika maandalizi ya msimu mpya,
imegundulika kuwa marejeo yangu dimbani yatachukua muda mrefu kuliko
tulivyotarajia na daima mimi napenda kufanya kilicho bora kwa faida ya timu,
ndio maana nimeamua kujiweka mbali," maelezo ya Frings kuhusu kujiuzulu
yalisema.
Akizungumzia uamuzi huo wa Frings, Meneja wa klabu hiyo,
Kevin Payne alisema: "Kila mmoja anampa pole Torsten na hawataweza jkumona
akiiongoza Toronto
msimu huu kutokana na kipindi kirefu cha majeraha na hapo ndipo tatizo lilipo."
"Tunautambua na kuukubali mchango wa Torsten kwa Toronto
FC na tueridhika na maamuzi ya awali ya kujiunga nasi akizikana klabu kadhaa
Ulaya," alimaliza Payne.
SuperSport.com
No comments:
Post a Comment