HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 28, 2013

RAFA BENITEZ: WACHEZAJI WANANIUNGA MKONO 100%

LONDON, England

“Ulikuwa mkutano baina ya wachezaji na benchi la ufundi kubadilishana mawazo na kusikitishwa ama kuchanganyikiwa ni kitu cha kawaida tu baada ya kipigo. Lakini naweza kuhakikisha kuwa wachezaji wako nyuma ya mawazo yetu kwa asilimia 100 katika kile tunachopanga na kujaribu kufanya”

KOCHA Rafael Benitez amesema nyota wa klabu yake ya Chelsea wanamuunga mkono na wako nyuma yake kwa asilimia 100 – licha ya kutoleanma lugha chafu na nahodha John Terry.

Benitez ameenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa, yeye ahofii kujeruhiwa kwa namna yoyote kutokana na uungwaji mkono anaopata kutoka kwa wachezaji wake.

Mhispania huyo, juzi usiku aliithibitishia SunSport taarifa kuwa alikuwa na mkwaruzano wa aina yake kwenye mazoezi ya kikosi chake baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Manchester City Jumapili iliyopita.

Benitez alisema: “Ilikuwa kubadilishana mawazo kwa ufupi mno na hivyo ndivyo ilivyokuwa.

“Ulikuwa mkutano baina ya wachezaji na benchi la ufundi kubadilishana mawazo na kusikitishwa ama kuchanganyikiwa ni kitu cha kawaida tu baada ya kipigo.

"Lakini naweza kuhakikisha kuwa wachezaji wako nyuma ya mawazo yetu kwa asilimia 100 katika kile tunachopanga na kujaribu kufanya.”

Katika malumbano yake na wachezaji, nahodha Terry alijitetea yeye binafsi na nyota anawaongoza, kutokana na shutuma na ukosoaji mkubwa waliokuwa wakipata kutoka kwa Benitez.

Kuumia kwa Gary Cahill na Cesar Azpilicueta, kulitarajiwa kungempa namba kikosi cha kwanza Terry katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Middlesbrough jana usiku, licha ya kutibuana na kocha wake huyo.

The Sun

No comments:

Post a Comment

Pages