HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2013

Hasira za Ndugai ndani na nje ya Bungeni


Na Bryceson Mathias

MWANAMKE aliyetambulisha kwa Jina la Mama Rehema, amemjia juu Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai akimtaka kushuka na kutenda haki anapoendesha vikao ndani ya Bunge na akiwa nje.

Mama huyo alisema hayo alipotoa mchango wa mawazo yake Jana katika kipindi cha Kipima Joto kilichorushwa moja kwa moja Televisheni ya ITV na kuendeshwa na Mtangazaji Winfred Masako, kilichohoji ‘Kanuni za kuendesha Bunge, Je zinajenga Demokrasia? 

Baada ya Michango ya wageni Waalikwa Naibu Spika Ndugai, Pasiance Mlowe, Tundu Lisu, Marcossy Albanie na michango ya Wanaanchi Mitaani, Masako aliporuhusu michango, Mama Rehema alisema,

“Yeye bado ni mtoto mdogo lakini kikweli huwa naona haki ya Kidemokrasia haitedeki, na Mhe. Ndugai kama kiongozi huwa  una Hasira sana unapoendesha vikao vya Bunge na kama kiongozi wa mfano unatakiwa ushuke, mfano sasa hivi kwenye ITV tunaone unaonesha Hasira kwa Lisu”.

Sawa na wachangiaji wengine, Mwaamke huyo alimwambia Ndugai, Wananchi wanaelewa na wanaona kila kinachotendeka ndivyo sivyo vikikosa Haki, kiasi kwamba wananchi wamechoshwa na yanayojiri bungeni na Kiti cha Spika kinavyotakiwa kifanye.

Kutokana na hali hiyo alisema, wananchi wamepoteza Imani na Matumaini ya Watawala wakiwemo Mawaziri na Bunge, kufuatia kukanywagwa kwa Kanuni hasa kwenye eneo la kuzitafsiri.

Awali Ndugai ambaye alikuwa hataki kuanzisha mdahalo huo akitaka waanze wengi ili yeye ajibu, alilazimishwa na Mtangazaji Masako, ambapo muda wote aliacha hoja na kumshambulia Lisu na Matamko ya Chadema Mwembe Yanga Temeke, huku  Lisu akionekana kupanga hoja kwa umakini.

Hata hivyo alisema, Kiti cha Sika kimetoa nafasi nyingi za kuchangia kwa wapinzani kuliko Chama Tawala, ambapo Albanie licha ya kulaumu ukiukwaji wa Kanuni Mamlaka ya Spika kuvunja Kamati, pia alilaani wabunge kutumia viba kodi ya wananchi akidai wamelipwa Mil. 321/- bila kufanya kazi kwa kutopitisha Muswada iliyoahirishwa, akitaka maelezo.

Aidha kwa upande wake Mlowe aliwaonya Wabunge wa  Chama Tawala wasiwe Serikali, na kuwataka wabunge wote bila kujali itikadi, wawatendee haki wananchi, wakumbuke wajibu wao, ambapo pia alidai hoja ya James Mbatia (NCCR-Mageuzi) Kuhusu Udhaifu wa Sekta ya Elimu haikuwa ya kubezwa.

No comments:

Post a Comment

Pages