DAR ES SALAAM, Tanzania
WAZIRI wa Nchi wa Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira), Dk Trezya Huvisa, amesema wizara hiyo, inatarajia kuanzisha
Kitengo cha Polisi ambacho kitasimamia utunzaji na kuwakamata wale wote
wataochangia uharibifu wa mazingira.
Huvisa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari, kuhusu maadhimisho ya
Siku ya Mazingira itakayofanyika Machi 3 mwaka huu kwenye viwanja vya
Tanganyika Parkers jijini.
Alisema kitengo hicho kitafanya kazi hiyo, ya
kuwadhibiti watu wanaofanya uharibifu wa mazingira kwa kushirikiana kwa karibu
na jamii ambayo inawatambua baadhi ya watu hao.
“Ni vyema tunapoazimisha siku hii tutafakari
kwa kina changamoto mbalimbali zinazochangia uharibifu mkubwa wa
mazingira”alisema.
Huvisa, alisema siku hiyo imetengwa kwa lengo
la kukumbushana juu ya umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira barani Afrika.
Aidha, kila mmoja wenu atumie fursa hiyo kwa
kuelimisha na kukumbshana kuhusu wajibu
wa kuyatunza mazingira kwa manufaa kila mtu na vizazi vijavyo.
“Ujumbe wa Siku ya Mazingira Afrika mawaka
huu ni Ushirikiano wa Nchi za Afrika katika ktekeleza dhana ya Uchumi wa
Kijani, ili kukuza uchumi na kuhifadhi
mazingira barani Afrika”alisema.
Vilevile alisema ujumbe huo unahimiza ushirikiano
wa kila mtu kutimiza wajibu wa kukabiliana na uharibifu wa mazingira
unaosababishwa na matumizi ya rasilimali yasiyoendelevu.
Huvisa alisema kwa mfano dhana ya uchumi wa
kijani inahimiza kila mtu kuhifadhi mazingira kwa kufanya shughuli za uchumi zisizoharibu
mazingira.
Alizitaja shughuli hizo kuwa ni pamoja na
kutumia nishati jadifu, majiko banifu, nishati mbadala, kupunguza uzalishaji wa
taka na kuhakikisha miji yote inakuwa safi.
Huvisa alitumia fursa hiyo, kwa kuwakumbusha
Watanzania wajibu wa kutii Sheria ya mazingira ya Mwaka 2004, kwa kila
mwananchi kuifahamu Sheria hiyo ya Mazingira na kuitekeleza inavyotakiwa.
No comments:
Post a Comment