HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2013

CRDB YATAMBIA TUZO YA SUPERBRANDS

  Mkurugenzi kutoka taasisi ya Superbrand, Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya Superbrands.
Baadhi ya wageni walio hudhuria tafrija hiyo.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza na waandishi wahabari juu ya sababu zilizoipaisha Benki ya CRDB hadi kutunikiwa cheti cha Superbrand kwa mara ya tatu mfululizo pia mikakati ya benki hiyo katika kuboresha huduma zake ili kuendeleza rekodi yake ya kupata cheti hicho kila mwaka.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB-Uendeshaji na huduma kwa wateja Saugata Bandyopadhyay (kulia) akipokea cheti cha Superbrand kutoka kwa mkurugenzi wa Superbrand, Jawad Jaffer.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB-Uendeshaji na huduma kwa wateja Saugata Bandyopadhyay wakati wa tafrija ya kupokea cheti cha Superbrands.


DAR ES SALAAM, Tanzania 

BENKI ya CRDB imetambia huduma za kisasa za kibenki inazotoa, zilizowawezesha kupata tuzo za Ubora wa Makampuni ‘Superbrands 2013/14’ kwa mwaka wa tatu mfululizo, ambapo imeahidi maboresho zaidi ili kuhakikisha inaendelea kufanya vema kitaifa na kimataifa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Wateja wa benki hiyo Tully-Esther Mwambapa, wakati akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands - Afrika Mashariki na Kati, Jawad Jaffer, kwenye Hoteli ya Kempinski.

Mwambapa alisema CRDB imefurahishwa kuwa moja ya makampuni yaliyotunukiwa tuzo hiyo kutoka Kituo cha Utafiti wa Viwango vya Ubora na Ufanisi Katika Huduma za Makampuni (TCBA), cha London, Uingereza na kwamba kwao ni changamoto ya maboresho zaidi katika huduma zao.

“CRDB inaichukulia tuzo hii ya Superbrands kama chagizo kuu la kuboresha huduma za kibenki, huku tukiamini kuwa itasaidia katika kutanua wigo wa maendeleo ya uchumi kitaifa na kimataifa, kutokana na ukweli kuwa benki hii kwa sasa imevusha huduma nje ya Tanzania,” alisema Mwambapa.

Aliongeza kuwa, katika kuhakikisha wanaendelea kuwa miongoni mwa makampuni yanayofanya vema na kutunukiwa tuzo hiyo kila mwaka, CRDB imejipanga kuitumia ipasavyo heshima waliyopewa na TCBA na wadau wengine, ambayo itachangia kuitangaza benki ndani na nje ya nchi.

Akizungumza wakati akikabidhi tuzo hizo, Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands, Jawad Jaffer, alisema kuwa vigezo mbalimbali vya ubora wa huduma vilitumika kuyapata makampuni bora na kuyataka kuzienzi tuzo kwa kuboresha utendaji wao kwa ustawi wa maendeleo ya wateja na taifa. 

No comments:

Post a Comment

Pages