Ukaguzi/picha ya pamoja; Vikosi vya Bayern Munich (kulia) na Arsenal muda mfupi kabla ya kuanza kwa pambano la marudiano 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena jana na Arsenal kuichapa Bayern 2-0. Hata hivyo Gunners imeng'olewa kwa sheria ya bao la ugenini.
Hakuna kuremba; Beki wa kushoto wa Arsenal, Kierran Gibbs, akimchezea rafu kiungo Mholanzi wa Bayern, Frank Ribery wakati wa mechi hiyo jana usiku.
Tunataka haki; Hapa ni mchezaji wa Bayern, Thomas Muller akilalamikia moja ya maamuzi wakati wa mechi hiyo.
Luis Gustavo wa Bayer (kulia), akijaribu kumkabili nyota wa Arsenal Santi Cazorla.
Kulalamikia maamuzi; Huyu ni Mfaransa anayeinoa Arsenal, Arsene Wenger, akinyoosha mikono juu kulalamikia moja ya maamuzi ya refa wa pambano hilo.
Jaribio tata; mlinda mlango wa Bayern akizongwa na wachezaji wa Arsenal, huku wale wa Bayern wakimuamulia, baada ya kuudaka mpira uliovuka mstari kwa nia ya kumdanganya mwamuzi kuwa sio bao. Hata hivyo mwamuzi alilikubali bao hilo la pili.
Ulinzi shirikishi; Javi Martinez wa Bayern (8), akijaribu kumzuia kiungo na nahodha wa Arsenal, Mikel Arteta katika mechi hiyo, huku beki mwingine wa Bavarians akiwa tayari kutoa msaada kwa Martinez.
Aaron Ramsey akiwa na mpira aliouokota nyavuni akishangilia bao la kwanza la Arsenal
Olivier Giroud (kushoto), akishangilia bao lake akiwa na winga Theo Walcott, aliyepiga pasi ya mwisho iliyozaa bao hilo.
Kitu kambani; Bao la kwanza la Gunners katika mtanange huo.
Mtiti langoni; Kipa wa Bayern akizongwa baada ya jaribio tata la kuudaka mpira uliotinga nyavuni.
Kiungo wa zamani wa Bayern Munich, Owen Hargreaves akifuatilia pambano la timu hiyo na Arsenal jana usiku akiwa jukwaani.
Beki wa kati wa Arsenal, Laurent Koscielny (wa kwanza kushoto), akipiga kichwa kuifungia timu yake bao la pili, ambalo halikutosha hata hivyo kuivusha Gunners kwenda robo fainali Mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment