Uche Unigwe Meneja Mkazi wa Heineken Tanzania akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja Biashara, Masoko wa Heineken Tanzania, Caroline Kakwezi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo akizindua mashindano ya mchezo wa Foosball jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
WADHAMINI wa Ligi ya Mabingwa
Ulaya ‘Eufa Champion League’ imezindua michuano ya mchezo mpya wa Foosball kwa
mashabiki wa ligi hiyo, ambako washindi watajikatia tiketi ya kusafiri nchini
Uholanzi.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa michuano hiyo katika Mgahawa wa Akem jijini Dar es Salaam jana,
Meneja wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe, alisema, michuano hiyo
itawashirikisha wateja wake hapa nchini, ikielekea kwenye harakati za mwisho za
wa msimu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2012/2013.
“Foosball, ni mchezo ambao
kwa wengine unajulikana kama ‘mpira wa mezani’, ni mchezo unaochezwa duniani
kote, ingawa mara nyingi zaidi ni kwenye baa na historia inaanzia mwaka 1923.
Katika mchezo huu wapinzani wanasimama pande zote za meza na wanajaribu kufunga
magoli,” alisema Unigwe.
Wanajaribu kuipiga mipira,
ambayo inaanzishwa kutoka ng’ambo nyingine ya meza, wakitumia fimbo
zilizotengenezwa na aluminium iliyounganishwa na sanamu za wachezaji wa mipira.
Mshindi anapatikana kwa kufunga magoli mengi zaidi, kwa kawaida huwa kuanzia
matano, 10 au 11.
“Michuano ya Foosball ni ya
kusisimua na itatengeneza tukio la kihistoria, ambapo wale watakaofikia fainali
watashindanishwa wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikioneshwa ‘live’
Mei 25 Dar es Salaam na watakaobuka mabingwa watashinda safari ya kutembelea
makao makuu ya Heineken jijini Amsterdam Uholanzi, wakilipiwa gharama zote,”
alisema.
Naye Mkurugenzi wa Heineken
Afrika Mashariki, Koen Morshuis, alisema; “Heineken inajitoa kuwapa wateja wetu
wa Afrika Mashariki tukio la kipekee kama ilivyokuwa katika ziara ya Kombe la
Ligi ya Mabingwa Ulaya 2012. Mwaka huu michuano ya Foosbal inalenga kuwapa
changamoto wateja wetu kuonyesha ujuzi na vipaji vyao,”.
No comments:
Post a Comment