HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 08, 2013

CCM YATOA TAMKO KUTEKWA NA KUPIGWA KWA KIBANDA



CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI  NDOGO YA MAKAO MAKUU  S.L.P. 9151 DAR ES SALAAM F2180108


 Barua zote zipelekwe kwa Katibu Mkuu                                               Fax: 255-022-2185245; 022-2184580

  

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku wa kuamkia Jumatano Machi 6, 2013.
Chama Cha Mapinduzi kinalaani kwa nguvu zote kilichotokea kwa Absalom Kibanda, kwani ni unyama usiokubalika hata kidogo, unafaa kulaaniwa na Watanzania wote.
CCM tunaitaka Serikali kuhakikisha inawapata waliofanya unyama huo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, na kukomesha matukio ya namna hiyo.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa Uongozi wa Jukwaa la Wahariri, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, familia ya Ndugu Kibanda, wanahabari na wadau wote wa habari nchini, na tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka na kurejea katika kazi zake za Ujenzi wa Taifa.

Imetolewa na:


KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UEENEZI
08/03/2013

No comments:

Post a Comment

Pages