Luis Nani wa Man United akimchezea rafu mbaya Alvaro Abeloa wakati wa mechi kati ya timu hiyo na Real Madrid
Nani akioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Cuneyt Cakir wa Uturuki.
Nani akishindwa kuamini kilichomkuta
Sir Alex Ferguson akilala kwa mwamuzi wa akiba kutokana na kadi nyekundu aliyooneshwa Nani.
Wachezaji wa Man United wakimtangulia mwamuzi Cuneyt Cakir anayesindikizwa na askari polisi.
MONACO, Ufaransa
Kadi nyekundu ya Luis Nani iliwatibua nyongo Man
United, ambapo ‘waliotoka’ mchezoni na kujikuta ikichapwa mabao 2-1
ilipowaalika Real Madrid, kabla ya Ferguson kususia mkutano
na vyombo vya habari
KAMATI ya Nidhamu ya
Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), iko katika mpango wa kuiadhibu klabu ya Manchester
United, kutokana na vinara hao wa Ligi Kuu ya England kuonesha utovu wa nidhamu
wakati wa mechi ya kichapo kutoka kwa Real Madrid Jumanne Usiku.
Bodi hiyo yenye mamlaka ya
kinidhamu katika shirikisho hilo,
inapanga kuijadili kadi nyenkundu ya moja kwa moja aliyooneshwa Luis Nani,
ikiwemo kususia mkutano na vyombo vya habari baada ya mechi uliofanyika ndani
ya dimba la Old Trafford.
Nani, nyota wa kimataifa wa
Ureno, alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Mturuki Cuneyt Cakir kunako
dakika ya 56 kwa kumkanyaga kifuani Alvaro Arbeloa wakati akiwania mpira.
Baada ya kadi hiyo iliyotoka
wakati United ikiongoza kwa bao la kujifunga la Sergio Ramos, wenyeji hao
wakapoteza dira na kujikuta ikichapwa mabao 2-1 na kutupwa nje ya michuano kwa
jumla ya mabao 3-2.
Sasa kadi hiyo ya Nani
itajadiliwa na kamati hiyo, kuweza kuona kama
itakuwa ya kifungo cha mechi moja, ama watamuongezea adhabu ya kukosa mechi
zaidi.
Kocha wa Man United, Sir Alex
Ferguson alikasirishwa na kadi hiyo na kuamua kususia mkutano wake na vyombo
vya habari, huku msaidizi wake Mike Phelan akichukua nafasi yake kuzungumza na waandishi.
Phelan alimtetea bosi wake
kwa kusema hayuko katika akili ya kawaida kuweza kuzungumza na akiwa mkutanoni
kwa niaba ya Mscochi huyo alisema: "Kuna taharuki kuu chumba cha kuvalia,
hali kaadhalika kwa kocha, ndio maana mimi niko hapa."
Uefa imesema kamati husika
itakutana kujadili na kutoa maamuzi juu ya yote yanayohusu mechi hiyo hapo
Machi 21.
Haijulikani kama beki wa
Mashetai Wekundu hao Rio Ferdinand, atakuwamo katika maamuzi ya kamati hiyo,
baada ya mlinzi huyo kumshutumu vikali Cakir baada ya filimbi yake ya kumaliza
mchezo, ambapo kundi la wachezaji wa United walimzonga mwamuzi huyo.
BBC Sport/The Sun
No comments:
Post a Comment