HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2013

UJENZI VIWANJA VYA KOMBE LA DUNIA 2014 WASUASUA

RIO DE JANEIRO, Brazil

IMEBAKI miezi mitatu kabla ya fainali za soka za Kombe la Mabara kuanza kutimua vumbi hapo Juni mwaka huu, takribani miezi 12 kabla ya Kombe la Dunia kurindima kwenye viwanja tofauti nchini Brazil.

Viwanja vingi viko katika matengenezo, ambayo kimsingi yametia shaka kama makamilisho yake yanaweza kutimia kwa wakati kuiwahi michuano yote miwili mikubwa zaidi duniani.

Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mabara 2013 na ile ya Kombe la Dunia 2014, karibu viwanja vyote ujenzi unaendelea na ufuatao ni muhtasari wa kiwango cha makamilisho ya viwanja hivyo.
Asilimia za makamilisho ya viwanja vya Kome la Dunia 2014 nchini Brazil uko kama ifuatavyo:  

Mane Garrincha (Brasilia) - umekamilika kwa 89%
Arena Corinthians (Sao Paulo) - umekamilika kwa 60%
Castelao (Fortaleza) - umekamilika na utazinduliwa Januari 2014 
Mineriao (Belo Horizonte) - Complete, but eventual occupancy is in dispute
Beira-Rio (Porto Alegre) - umekamilika na utazinduliwa Septemba 2013
Arena Fonte Nova (Salvador) - umekamilika na utafunguliwa mwisho wa mwezi huu
Arena Pernambuco (Recife) - Umekamilika kwa 90%
Arena Pantanal (Cuiaba) - umekamilika kwa 60%
Arena Da Amazonia (Manaus) - umekamilika kwa 50%
Arena Das Dunas (Natal) - bado uko katika matengenezo ya awali (unatia shaka kukamilika kwa wakati
Arena Da Baixada (Curitiba) - umekamilika kwa 55%
  Huu ndio uwanja mkubwa zaidi Brazil uitwao Maracana baada ya kubomolewa kwa lengo la kuufanyia maboresho kwa ajili ya Kombe la Dunia 2014. Wajezi wa uwanja huu waaaligoma kushinikiza mambo kadhaa ikiwamo bima kwa na familia zao, pamoja na ongezeko la mishahara na vyakula kazini. Miezi micahache sasa kabla ya kuanza kwa Kombe la Mabara, Uwanja huu haujakamilika, huku miezi 15 ikiwa imesalia kabla ya Kombe la Dunia mwakani.
 Sehemu tu ya madimbwi ya maji katika ujenzi wa uwanja wa Maracana, huku mabomba ya kunyonya maji yakijaribu kupunguza maji hayo ili ujenzi uendelee.
 Draja dogo nje ya uwanja lipitishalo mashabiki kuingia uwanjani, likipita juu ya bwawa kubwa la maji yanayodumaza harakati za ujenzi wa uwanja wa Maracana.
Uwanja pekee ambao umekamilika kwa asilimia 100 ni huu wa Mineiro. Brazil inahaha kumaliza viwanja hivyo kwa wakati ili kuwahi fainali za Kombe la Mabara 2013 na Kombe la Dunia 2014.
Uwanja pekee ambao umekamilika kwa asilimia 100 ni huu wa Mineiro. Brazil inahaha kumaliza viwanja hivyo kwa wakati ili kuwahi fainali za Kombe la Mabara 2013 na Kombe la Dunia 2014.

No comments:

Post a Comment

Pages