TANGA, Tanzania
Mshambuliaji Simon Msuva wa klabu ya Mabingwa wa Soka
Afrika Mashariki na Kati Yanga, leo ameendeleza mpango wake wa kufunga walau
bao 1 katika kila mechi lala salama ya ligi kuu Tanzania Bara.
Msuva aliiambia Habari Mseto hivi karibuni kuwa, hatahakikisha
mechi zote zilizobaki anafunga ili kuendeleza mikakati yake na malengo ambayo
amejipangia katika ligi hii 2012/13 inayofikia ukingoni Mei 18 mwaka huu.
“Namshukuru mungu nilichokipanga katika mechi hizi
zilizosalia kwa sasa nimekifanikisha hata leo katika mchezo wetu na Mgambo JKT
nimefunga japokuwa tumetoka sare, ya bao 1-1 eheee mungu nisaidie,”amesema.
Mchezaji huyu aliyetua Yanga akitokea Moro United ilishuka
daraja msimu uliopita, amekuwa mwiba katika timu yake na kuwapa presha baadhi
ya washambuliaji katika timu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Twiga na Jangwani
Kariakoo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment