HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 14, 2013

Chadema yavuna 150 Ngh’umbi-Kongwa



Na Bryceson Mathias, Ngh’umbi - Kongwa

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Ngh’umbi  Wilaya ya Kongwa, Kimevuna Wananchama 150 katika Kampeni ya Mabadiliko (M4C), yaliyoanzishwa na Viongozi wa juu mkoani Dodoma, baada ya kuzindua Kanda ya Kati, inayounganisha Mikoa ya Morogoro,Singida na Dodoma.

Wananchama hao wamepatikana katika Vijiji  Vitatu (3) vya Ngh’umbi, Mbagilwa na Mhongwa, ambapo viongozi wa muda walisema tayari Matawi matatu yameasisiwa,  na sasa yanasubili Viongozi wa Kitaifa wa Chadema walioko bungeni, wafike kuyafungua na kufanya Mikutano ya Nguvu..

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Mwenyekiti wa Mpito Kata ya Ngh’umbi, Boaz Sebai alisema, Mafunzo ya Elimu kwa wananchi kwa ajili ya Kuunda Matawi ya Chama na kuweka Viongozi (Mabalozi) yaliyoendeshwa na Chama Dodoma , yamewapa akili kiasi cha kuvuna wanachama wengi.

“Tuliendesha Mabadiliko ya M4C Nyumba kwa Nyumba, Mtaa kwa Mtaa, Kijiji kwa Kijiji na kufanikiwa kuvuna Wanachama 150 na tuna Mabalozi  kila baada ya Nyumba 10, na Matawi Matatu yameandaliwa kwa Ufunguzi “.alisema Sebai.

Sebai amesema, kazi  ya kuwakomboa watanzania inaendelea katika vijiji vingine ila tu wameishiwa na vifaa vya Uanacha zikiwemo na Bedera, ambazo Uongozi wa Wilaya umeahidi kuwapatia mara tu zikiwasiri kutoka Ofisi za Mkoa na zikikosekana zitaombwa Ofisi za Taifa Dar es Salaam.

Mwenyekitii wa Chadema Wilaya ya Kongwa Juma Juma Chibiriti, amethibisha kuvuna  wananchama hao waliojiunga na Chadema katika Kampeni ya Mabadiliko (M4C) ya Nyumba kwa Nyumba, Mtaa kwa Mtata na Kijiji kwa Kijiji, na kusema kusema, Mbinu hiyo ni Mzuri kwa Mafanikio ya Chama.

Aidha alisema anaasiliana na Viongozi wa Kitaifa walioko bungeni, waweze kwenda katika maeneo hayo ili wakafungue Matawi hayo na kuwashukuru wananchi kwa kuthubutu kufanya mabadiliko ya kimfumo, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na Kimaendeleo wilayani kwake.

No comments:

Post a Comment

Pages