HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 14, 2013

Pinda achangia Umoja wa Kinamama KKKT Mizinga 100 ya Nyuki



Na Bryceson Mathias, Ndzuguni Dodoma
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Peter Pinda, Jumapili, Mei 12, aliuchangia Umoja wa akina Mama wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mizinga 100 ya nyuki na kuahidi kuwachimbia Kisima.
 
Pinda alitoa ahadi hiyo alipozindua Mradi wa Nyuki wa Umoja huo ulioko Nduguni nje kidogo ya Mji, ambapo aliwataka Maafisa Mifugo kuwatafutia eneo la lingine la Eka Tano ili wafuge Kuku na Kulima Mbogamboga na Matunda  kwa eneo walilonalo ni Dogo.
 
Akizundua Mradi huo wenye Wanachama 50 na Mizinga 51, Licha ya kuwachangia Mizingo 100 yenye thamani ya Mil. 6,000,000/- kila Mzinga Sh. 60,000/-, Pinda aliahidi kuwachimbia Kisima ili kuwawezesha kupata Maji, ambapo aliziagiza Taasisi za Kiraia na Madhehebu ya Dini kuanzisha na kuendeleza Vikundi vya wafugaji Nyuki nchini maana wanalipa.
 
“Taasisi za Dini na Madhebu ya Dini, anzisheni na kuendeleza vikundi vya wafugaji nyuki nchini, lengo likiwa ni kupata Asali na Nta kwa vile ni njia rahisi ya kuwaongezea wananchi vipato na kupunguza Umaskini.
 
“Nyuki hawana gharama kama Kilimo au Ufugaji mwingine, Wanahitaji Maji, Mimimea inayotoa Maua na Nyumba ya kuishi (Mizinga) ya Kisasa ya Mbao, Watakutengenezea Asali nyingi ambayo sasa ina Soko na bei nzuri ndani na nje ya nchi”.
 
Ni sisi waswahili hatuthamini Ufugaji wa Nyuki, lakini Ulaya na Marekani , ingawa kuna Mazingira Magumu ya ya Baridi kwa ufugaji wa Nyuki, wanafugha sana tena kwa kuipanga Mizinga chini”.alisema Pinda.
 
Mchango wa Pinda unatokana na risala yao iliyosomwa na Mwenyekiti wao suzani Chekani iliyoainisha changamoto wanazopata katika Mradi wao, mojawapo zikiwa ni Eneo, Mitaji, Maji, Vifungashio, Vifaa vya Kulinia Asali,  Mitaji ya kununulia Mizinga, Uelewa na Mabanda, huku ukiwa na Matarajio ya kuwa na Mizinga 500 na kushiriki maadhimisho ya Nanenane.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Dayosisi ya Dodoma KKKT Askofu Amoni Kinyunyu, alimshukuru Pinda kwa kutumia Muda wake kufika na kuzindua Mradi huo, akimpongeza kwa kuthamini Mchango wa akina Mama hao wa Kanisa wa kuliletea pato Taifa, ambapo wanawake hao walijifunza ufugaji huo kwenye Shamba darasa la Nyuki la Pinda Zuzu.

No comments:

Post a Comment

Pages