HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 15, 2013

FAINALI EUROPA LEAGUE: NI KIAMA CHELSEA VS BENFICA LEO



LONDON, ENGLAND 

"Hakika, Chelsea inapewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa kutokana na ughali wa kikosi chake na uzoefu wa wachezaji, lakini kwa maoni yangu, kimbinu, wachezaji wa Benfica ni bora zaidi kuliko wa Chelsea"

BENFICA ya Ureno, inaingia dimbani leo katika fainali ya Europa League ikiwa na kilicho kamili kila idara kuliko wapinzani wao Chelsea, ingawa hawapewi nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, hii ni kwa mujibu wa Sven-Goran Eriksson

Chelsea, inashuka ndani ya Dimba la Amsterdam Arena jijiji Amsterdam, Uholanzi, katika fainali yake ya pili mfululizo ya michuano ya klabu barani Ulaya, huku ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Eriksson, kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England ‘Three Lions,’ anafahamu mengi kuhusu Benfica, baada ya kuwa ameshawahi kufanya kazi na mabingwa hao mara mbili mfululizo wa soka barani Ulaya.

"Hakika, Chelsea inapewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa kutokana na ughali wa kikosi chake na uzoefu wa wachezaji, lakini kwa maoni yangu, kimbinu, wachezaji wa Benfica ni bora zaidi kuliko wa Chelsea," alisema Eriksson kuliambia gazeti la aBola.

"Kimbinu Benfica ni kikosi hatari sana. Wanajua kumiliki vema mpira na kucheza soka safi mchezoni," aliongeza Mswedeni huyo.

Mabingwa hao wa Ulaya miaka ya 1961 na 1962, wako imara wakiwategemea viungo wake mahiri Eduardo Salvio, Nicolas Gaitan, Pablo Aimar, Ola John na Nemanja Matic, kuzalisha mpira kwa mtikisa nyavu wake Oscar Cardozo.

Cardozo, anayewezeshwa katika jukumu la ufungaji na wasaidizi wake Lima na Rodrigo, kwa pamoja wakali hao wamefunga jumla ya mabao 71 katika mechi 118 walizocheza msimu huu.

Eriksson, ambaye alikuwa kocha wa Benfica wakati wakichapwa bao 1-0 na AC Milan katika fainali ya Kombe la Ulaya mwaka 1990, jijini Vienna, Australia, anaamini Wareno hao watasahau kichapo cha mabao 2-1 ilichopata Jumamosi iliyopita dhidi ya FC Porto.

"Fainali ya Ulaya ni jambo la kuvutia," alisema Eriksson na kuongeza: "Mapema sana walishaanza maandalizi ya fainali hii na mechi dhidi ya Porto ilikuwa ni kuiweka sawa kiakili tu."

Mwamuzi wa mpambano huu ni Mholanzi Bjorn Kuipers, ambapo mshindi ataumana na mshindi wa fainali ya Mabingwa Ulaya kati ya Bayern Munich na Borussia Dortmund – kuwania ubingwa wa Super Cup kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa michuano ya klabu Ulaya.

Supersport.com

No comments:

Post a Comment

Pages