Roberto Mancini
MANCHESTER, England
Kocha Msaidizi Brian Kidd, atakiongoza kikosi hicho
kuelekea mwisho wa msimu huu na baadaye ziara ya maandalizi ya msimu ujao,
itakayofanyika huko Marekani kuanzia mwishoni mwa mwezi huu
HATIMAYE Roberto Mancini juzi usiku alifukuzwa rasmi kazi ya
kuinoa Manchester City, takribani mwaka mmoja tangu alipoiwezesha klabu hiyo
kuvunja mwiko wa miaka 44 ya kutotwaa taji la Ligi Kuu ya hapa.
Klabu hiyo yenye makao yake makuu kwenye dimba la Etihad,
ilisema: "imeshindwa kufikia malengo yake ndani ya uwanja, licha ya kuambulia
kufuzu michuano ijayo ya Ligi ya Mabinmgwa Ulaya."
Kocha msaidizi Brian Kidd, anakamata rasmi hatamu za uongozi
kuelekea mwisho wa msimu huu na ziara ya kikosi chake kwa ajili ya maandalizi
ya msimu ujao huko Marekani inayoanza mwishoni mwa mwezi huu.
Kocha wa Malaga, Manuel Pellegrini raia wa Chile, anatajwa
kuwa ndiye mrithi anayetarajkiwa kutangazwa kujaza pengo la Mancini, anayedaiwa
kujiandaa kuingia mkataba wa kuinoa AS Monaco ya Ufaransa.
Jumapili usiku, Pellegrini, 59, ambaye alitumia msimu mmoja
wa 2009/10 akiinoa Real Madrid, alikana taarifa kuwa kuna mazungumzo baina yake
na City ya kumrithi Mancini na kuwa kocha mpya Etihad.
Man City katika taarifa yake kuhusu kutimuliwa rasmi kwa
Mancini, 48, ilimshukuru Mtaliano huyo kwa kazi nzuri aliyoifanyia klabu hiyo
tangu alipojiunga Desemba 2009.
Lakini klabu ilisema kushindwa kufanya vema kufiki ‘malengo
maalum’ na haja ya klabu "kuendeleza mfumo chanya wa masuala ya jumla
yahusuyo soka Etihad," vimechangia kumfukuzisha kazi.
Hiyo inamaanisha kuwa, msamiati wa ‘masuala ya jumla
yahusuyo soka’ umeangalia mambo mengi kuizunguka klabu, na si dawati la ufundi
na chumba cha kuvalia pekee, bali pia inahusisha kwa mfano mfumo wa soka la
vijana – kuelekea kikosi cha wakubwa.
"Rekodi ya Mancini inaongea yenyewe, akiwa hapa alipata
upendo na heshima kubwa kutoka kwa mashabiki," alisema Mwenyekiti Khaldoon
Al Mubarak na kuongeza: "Alifanya vema kama alivyoahidi na alifanikiwa
kutwaa medali na mafanikio mengine."
Mancini aliyetua Etihad kujaza pengo la Mark Hughes, amedumu
klabuni hapo kwa miaka mitatu na nusu akiiwezesha klabu hiyo kutwaa Kombe la FA
mwaka 2011 na ubingwa wa Ligi Kuu mwaka jana – miaka 44 tangu ilipotwaa kwa
mara ya mwisho.
Baada ya ubingwa huo, Julai 2012, Mancini alisaini mkataba
wa miaka mitano ya kuendelea kutumikia klabu hiyo, ambao sasa City imeuvunja na
kumlipa kitita chake.
Badala yake ameambulia kuvuliwa ubingwa na majirani zao Manchester
United, huku akiaga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuichapwa
fainali ya FA Jumamosi iliyopita mbele ya vibonde wa Ligi Kuu wanaoshuka daraja
Wigan.
BBC Sport
No comments:
Post a Comment