Novak Djokovic akirudisha mpira kwa mpinzani wake Grigor Dimitrov (hayuko pichani, katika mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Madrid Open 2013 juzi.
MADRID, Hispania
Dimitrov, anayekamata nafasi ya 28 ya ubora duniani, halikuwa hajawahi kushinda hata seti (achilia mbali mchezo) dhidi ya Djokovic katika mara mbili walizowahi kukutana, lakini juzi alikuwa kwenye kiwango cha juu na kushinda kwa 7-6 (8-6) 6-7 (8-10) 6-3
KINARA wa viwango vya dunia vya ubora katika mchezo wa
tenisi, Novak Djokovic, juzi ameshangaza mashabiki wa mchezo huo kwa kukubali
kichapo katika raundi ya pili ya Michuano ya Wazi ya Madrid ‘Madrid Open 2013’
dhidi ya Grigor Dimitrov.
Dimitrov, anayekamata nafasi ya 28 ya ubora duniani, halikuwa
hajawahi kushinda hata seti (achilia mbali mchezo) dhidi ya Djokovic katika
mara mbili walizowahi kukutana, lakini juzi alikuwa kwenye kiwango cha juu na
kushinda kwa 7-6 (8-6) 6-7 (8-10) 6-3.
Nyota huyo wa kimataifa wa Bulgaria, mwenye miaka 21, alionekana
kumkabili vema Djokovic katika mechi hiyo na licha ya kushindwa kupata ushindi
katika seti ya pili, kila mmoja aliona umakini aliokuwa nao na kujua.
Akizungumzia ushindi huo, Dimitrov alisema: "Ulikuwa
ushindi mikubwa kwangu mimi. Najua lilikuwa jambo kubwa, bila shaka, lakini
unahitaji kukaa tayari mchezoni.
"Ni matumaini yangu kwamba unapaswa kujiweka tayari
kukabiliana na nyota kama huyu kwa miaka yako mchezoni. Ndio mechi ilivyo. Huwezi
kujua namna gani hali ya mambo itakuwa mnapokutana mara nyingine."
Djokovic, ambaye alitwaa taji la tatu kwa mwaka huu
aliposhinda ubingwa wa Monte Carlo Masters mwezi uliopita, alilazimika kutibiwa
jeraha la enka alilopata katikati ya seti ya pili ya mpambano huo.
BBC Sport
No comments:
Post a Comment