Juu: Logo ya 'Washika Bunduki' Arsenal FC. Chini: Mashabiki wa soka nje ya Uwanja wa Emirates jijini London, unaomilikiwa na Arsenal
LONDON, England
Mkataba wa sasa wa Arsenal na Kampuni ya Nike, wenye thamani ya pauni milioni 55 kwa miaka saba – unafikia tamati mwishoni mwa msimu ujao
KLABU ya Arsenal, imeingia mkataba wa jezi na vifaa vya
michezo na Kampuni ya Puma wenye thamani ya pauni milioni 170, unaohitimisha
miaka 20 ya Washika Bunduki hao kuvalishwa na Kampuni ya Nike.
Mtendaji Mkuu wa Gunners, Ivan Gazidis ametiliana saini na
Puma ya kuivalisha Arsenal kwa miaka mitano, mkataba unaomaanisha kuwa klabu
itapokea vifaa vyenye zaidi ya pauni milioni 30 kwa mwaka.
Mkataba wa sasa wa Arsenal na Kampuni ya Nike, wenye thamani
ya pauni milioni 55 kwa miaka saba – unafikia tamati mwishoni mwa msimu ujao.
Arsenal imekuwa ikikataa mikataba ya muda mrefu tangu
ilipohamia kwenye dimba la Emirates kutoka lile la zamani la Highbury mwaka
2006.
Lakini sasa imeanga mbele na kujaribu kutanua wigo wa
miakataba mipya na yenye tija.
Nike ilikuwa ya kwanza kukataa makubaliano ya mkataba mpya
Gunners, na kuamua kutofanya maboresho na nyongeza ya mkataba wa sasa.
Gunners inayonolewa na Arsene Wenger, ilitangaza na kufuata
sera za kubana matumizi yake kwa kila msimu, tangu ilipohama Highbury, miaka
saba iliyopita.
Sera hiyo inapingwa na mashabiki wa timu hiyo, wanaoumizwa
na ukame wa mataji wa miaka minane sasa, na wanaona timu yao inaweza kushindana
na klabu zinazotumia pesa kubwa England za Man United, Man City na Chelsea
kupitia pesa za udhamini.
The Sun
No comments:
Post a Comment