Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya polisi wa Kituo
kidogo cha Sitakishari Ukonga wailayani Ilala wanadaiwa kuacha kumfungulia
jalada la kesi mwizi wa viroba 71vya unga wa sembe, kumjeruhi muuzaji wa duka la
unga huo, baada ya kudaiwa kupokea rushwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Victoria Mwasonya, alisema tukio hilo lilitoke
kwenye duka la Mwera Super Sembe wiki iliyopita, Pugu Kaujiungeni (Kona).
Alisema mtu huyo (jina
tunalo), alifika dukani hapo akiwa na gari ghafla alianza kumshambulia kijana
aliyetajwa kwa jina moja la Jonas, mara baada ya kumjeruhi alipakiza unga huo
na kuikimbia kusikojulikana hata hivyo baada ya taaria hizo kufika polisi mtu
huyo alikamatwa.
Mwasonya alisema baada ya
kufikishwa kituo cha Polisi Sitakishari, katika hali ya kushanaza paoja PF3 kuonyehsa kuwa mtu huyo alimjeruhi
vibaya Jonas bado askari hao walishindwa kumfungulia kesi, huku wakishindwa
kutoa maelezo ya kuridhisha kwa husika.
“Kwanza mimi nashangaa
hata lile gari lililohusika kubeba mifuko ya unga wa wizi wameliachia bila
yakutueleza sasa tukifika mahakamani watambuwe kuwa nao ni wezi kwa kuwa
wamemsaidia mwizi kubeba vile viroba kwani hangeweza kuvibeba pekee
yake”alisema Mwsonya.
Mwasonya alisema
anaushahidi wa jina la askari aliyemtaka atoe rushwa ili asaidiwe kupata haki
yake, lakini alipokataa kufanya hivyo alitakiwa aondoke kituoni hapo, pamoja na kijana wake
wakati huo akiwa bado yuko hospitalini matokeo yake ni hayo.
Alipotafutwa mkuu wa kituo
hicho (OCS), Mary Saria kulitolea ufafanuzi suala hilo alisema kuwa hangeweza
kulizungumzia kwa kuwa wakati huo alikuwa kwenye daladala.
Naye Jonas ambaye ni
mpelelezi wa tukio hilo alisema suala la jalada la mtuhumiwa huyo aulizwe
mkubwa wake kwani yeye hana haki ya kulizungumzia hilo.
Naye Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ilala Marietha Minangi, alisema hajalipata tukio hilo bali aliomba
mwandishi ampe namba ya mlalamikaji ili awasiliane naye kwa taarifa zaidi kitendo
ambacho mwandishi alikitekeleza.
Hata hivyo, mwandishi
alipomtafuta tena majira ya saa 8:15 mchana simu yake iliita bila kupokelewa
wakati namba hiyo alipewa majira ya asubuhi.
No comments:
Post a Comment