Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imetakiwa kujenga
utawala bora katika kusimamia rasilimali kama vile madini, mafuta na gesi
asilia kwa lengo la kuwanufaisha wananchi.
Akizungumza na wandishi wa
habari katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti matumizi ya rasilimali hizo, Mjumbe
Jumuiya ya Taasisi ya ‘Revenue Watch’ Silas Olan’g, alisema utafiti huo
ulifanyika katika nchi 58 duniani.
Alisema imebainika kuwa
bado kuna changamoto mbalimbali katika kusimamia rasilimali hizo, serikali kutokuwa
wazi kwa wananchi kuhusu matumizi ya rasimali hizo.
Olan’g alisema katika
ripoti ya mwaka 2010 kuhusu usimamizi wa rasilimali hizo Tanzania ilikuwa ya
tano kati ya nchi zaidi ya 30 za kiafrika ambapo safari hii imekuwa ya 27 kati
ya 58.
Alisema kutokana na nafasi
hiyo inaonesha kuwa mwaka huu wa 2013 imeweza kupiga hatua katika utawala bora pamoja
usimamizi rasilimali hizo.
Hata hivyo, alisema bado
nafasi hiyo si ya kujivunia kwani iko kwenye eneo dhaifu, hivyo bado juhudi
zinahitajika katika kuongeza uwazi wa kutoa taarifa.
Olan’g alisema ripoti hiyo
pia imeonelea kuwa kuna ulazima kwa watunga sera kutunga sheria ya uhuru wa
habari ambayo itamlazimisha mwenye taarifa kuwapatia wananchi habari inayohusu
usimamizi wa rasilimali hizo.
“Kama inavyofahamika kuwa
ukimya wakutokuwa wazi na kutoa taarifa kwa jamii hali hiyo inatia shaka kwani
ifahamike usiri ni sawa na kichaka cha rushwa”alisema Olan’g.
Naye mgeni rasmi Askofu
Munga aliitaka serikali kuhakikisha inasimamia rasilimali hizo kwa ajili ya
jamii kwa ujumla na si kwa kikundi cha watu wachache.
“Uanajua tangu serikali
hii imeingia madarakani haijawafanyia chochote jamii zaidi ya kujiandaa na
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015”alisema Askofu Munga.
Alitoa wito kwa viongozi
wa serikali kuwa pindi wapatapo nafasi yakwenda nje ya nchi kujifuza jinsi nchi
za wenzao zilivyoweza kupiga hatua katika usimamizi wa rasilimali hizo lazima waweke maslahi na uzalendo kwa ajili
ya Taifa na si kujali posho tu.
No comments:
Post a Comment