Na Bryceson Mathias, Dodoma
SHEKHE wa Msikiti wa Nunge, mjini hapa, Shabani Kitilla, amewajia juu watawala na Viongozi wanaopotosha ukweli, akipinga kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) si Chama cha Kikristo, Kikabila au Kiukanda.
Kitilla alisema hayo jana slipohojiana na Gazeti hili, alipotakiwa kutoa msimamo wake kama Vurugu zinazodaiwa za kidini zinaoendelea kutokea nchini, yakiwemo matamko ya wanasiasa wanaoshindana kisera, ambapo wengine wakishindwa hudai Chama cha mwenzake ni cha Kidini, Kikabila na Kiukanda.
Akijibu Maswali, Kitilla alisema, Kama Viongozi wa Dini wanavyowafahamu waumini wanaozingatia Sala, Ndivyo wanavyowafahamu wanasiasa na Vyama vyao walivyo, maana Wanasiasa hao ni waumini wao, lakini Chadema si Kikristo, Kikabila au Kiukanda kama kinavyotajwa, mbona wamo Wa-Islamu?.
“Kama Chadema Kingekuwa hivyo, Basi Msajili wa Vyama kabla ya kushitakiwa alitakiwa aachie Ngazi maana alikiuka Sheria za kusajili Vyama na amekiacha hadi kiwe na Wabunge 48, basi ana matatizo” alisema Kitilla akiuliza, Waislamu na makabila mengine waliomo ni nani?.
Kitilla aliongeza, Uongo huo ndio uliopandwa kwa Chama cha Wananchi (CUF),Ukaota, ukamwagiliwa mpaka mavuno yakavunwa kwa sababu kilikuwa kinaimalika. Lleo Uongo uleule ndio unaotaka kutumika kuwapumbaza watanzania; Ninachoamini, mtu hadanganywi mara Mbili.; Watawala waache Hila!
Kuhusu Udini alisema, “Tunapougua na kuhitaji damu tunauliza ni ya Dini ya Kikristo au Mu- Islamu? Je Hewa tunayovuta tunauliza ni ya Mkristo au Mu-Islamu? Nawashauri Wakristo na Wa-Islamu wasidanganywe, Amani yetu ikatoweka kwa sababu ya watu wachache wenye Uroho wa Madaraka.
Aidha Kitilla aliyetaja namba zake 0754-512347 alidai, anawatafuta Viongozi wakuu wa Chadema wasio Wakristo, Mbunge Said Arfi, Zitto Kabwe (MP), Prof. Abdalah Safari, Halima Mdee (MP), Hamad Yusuph, Issa Mohamed na wengine, ili awaulize Chadema kuna udini? Wakisema hakuna atajiunga nao!
No comments:
Post a Comment