HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 13, 2013

Tendwa usiwe Kigeugeu


Na Bryceson Mathias
 
LICHA ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini, John Tendwa kusema hoja nyingine zinazotolewa na vyama vya upinzani ni za msingi na zinatakiwa kufanyiwa kazi. Wananchi wa Kada mbalimbali nchini, tunamtafsiri Tendwa kuwa kigeugeu.
 
Tendwa huyu huyu siku za hivi karibuni alikuwa akiviandama vyama vya upinzani na hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiasi cha kukitolea vitisho akidai anaweza kukifuta na kukiondoa katika usajili wa vyama vya siasa.
  
Niijiuliza na kushangaa kama Tendwa ndiye aliyetoa Kauli hii “hoja nyingine zinazotolewa na vyama vya upinzani ni za msingi na zinatakiwa kufanyiwa kazi”.alisema Tendwa.
  
Kauli ya Tendwa imekuja ikiwa imebaki miezi miwili ili Tanzania itimize miaka 21 tangu iingie katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, ambapo Tendwa alijigamba akisema,.
 
“Katika kipindi cha miaka 21, vyama vya upinzani vimeimarika na viongozi wake wametoa hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa, huku akisisitiza kuwa kama vikisema ukweli unatakiwa kufanyiwa kazi na siyo kubezwa” alisema Tendwa.
 
Kwa upande wangu kutokana na sintofahamu iliyokuwepo, sikutegemea Tendwa atasema Demokrasia imekuwa kwa kiwango kikubwa hali akitolea mfano mvutano kati ya CCM na CHADEMA, akidai unatakiwa kuchukuliwa kama mgongano wa kisiasa na si vinginevyo.
 
Sielewi kwa nini alimung’unya maneno aliposema, “Kikubwa ambacho viongozi wa chama Tawala na wale wa upinzani wanatakiwa kujihadhari nacho, ni lugha za matusi na kujihusisha na mambo ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani”. Lakini hakutaja kwamba baadhi ya Wabunge wa CCM wanaongoza kwa kutoa matusi.
 
Kama Tendwa anaelewa hata nchini Marekani, Chama cha Republican na Democratic vina upinzani mkali na wakati mwingine viongozi wake hurushiana maneno ya hapa na pale na kwamba, hivyo ndiyo siasa za vyama vingi, kwa nini kuna wakati anabungua Demokraia?
 
Namtaka Tendwa aamue moja kama Biblia Ufunuo wa Yohana 3:15-16Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
 
Watalaam wa Semi wanadai kwamba, Tafsiri ya Chakula kizuri ni Afya. Tendwa pamoja na kwamba hapo awali ulikuwa unaviuma vyama vya upinzani na hasa CHADEMA, naona sasa umeanza kupulizia jambo ambalo halina Afya maana tafsiri ya chakula ilikuwa kuwashakoo ya Demokrasia mnayoinadi.
Kama Chadema na Vyama vingine vimefikia hapo ulipoona vimefika, basi hiyo ni juhudi yao binafsi kisiasa, lakini (Tendwa) kama Msajili wa Vyama vya Siasa, hukuchangia chochote kukuza Demokrasia, bali kwa kuvipa vitisho vya  kuwafutia Usajili, ulikuwa unadumaza, unamong’onyoa  na kuua Demokrasia.
Adha sishangai kwa kile kilichokuwa kinatokea wakati wa michakato na shughuli za kisiasa, ambapo nyakati nyingine kama Mwamuzi , uliuma Filimbi badala ya kupuliza, ukaachia wanasiasa wapigane viatu. Lakini ninachojua mimi, Msiba ni Msiba tu ila Uombolezaji wake ni tofauti.
Maskini na Mlalahoi akiunguliwa kupata adha, hawezi kulia Kilio cha Tajiri au mwenye nacho. Wakati Mlalahoi kilio chake kinakuwa na makunyanzi, aliye nacho uso wake huwa laini ingawa machozi yanatoka. Hivyo; Tendwa usiwe Kigeugeu.
Pamoja na Siri kubwa ya Mbwa Mwitu wakila nyama, ni lazima wafute midomo  ili kuondoa Damu. asipojifuta, wenzake humshambulia na kumfanya Kitoweo.
0715933308

No comments:

Post a Comment

Pages