HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2013

Tusemeje Juu ya Bunge letu, Limelaaniwa?

Na Bryceson Mathias
 
BUNGE ni moja ya vyombo vitatu vikubwa na muhimu sana nchini, yaani Utawala, Mahakama na Bunge, ambavyo vinaheshimika kwa kiwango kikubwa kwa sababu kinabeba dhima kubwa ya kitaifa na kimataifa.
 
Lakini katika siku za hivi karibuni, Bunge kama Chombo kinachosababisha Utawala na Mahakama viboreshe na kutekeleza maagizo yake, kimeonekana si lolote si chochote, kutokana na mahali walipo kuonekana kama Klabu ya Pombe.
 
Bunge letu linalopaswa kuwa na Heshima Nene, halipaswi liwe na Kauli Nyafunyafu zinazotoa maneno Uzushi, Uhuni, Uzandiki, Uongo, Ushenzi, Mimba zisizotarajiwa, na yale ya siongei Mbwa naongea na mwenye Mbwa, apigwe, Msagaji mwenyewe na kadharika.
 
Awali Wabunge walipoanza, tulidhani bado wageni wa uelewa wa taratibu na Shughuli za Bunge, lakini pia tulidhani pengine ni mhemko wa kutofahamiana baina ya Mbunge na Mbunge, na pia tulidhani wakongwe wantaka vijana wawatambue ili wawaheshimu.
 
Cha kusikitisha, tulishuhudia Wakongwe na Wageni kama Juma Nkamia aliyetoka kwenye chombo kilichobobea maadili, na mwenzake  Livingstone Lusinde, anayotoka kwenye Familia inayoheshimika, ndio walioanza kutoa matusi, na ikatusikitisha sana.
 
Mahali lilipofikia Bunge sasa, Wananchi hata mimi, tunajiuliza Je, Bunge letu, Limelaaniwa? Nani aliyelilaani kama si Mungu Mola wetu? Kitu limekosa, hadi Mungu akafikia kulilaani, kiasi cha kudharirika kwa wanananchi Kitaifa na kimataifa?
 
 
Jambo la Pili, ni Mithali 27: 26 “Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri; Wala si kwema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao”. Wananchi wanaadhibiwa na kwa Gharama ya maisha na kunyang’anywa mali zao mchana kweupe, huku Wawekezaji wakiwadhulumu wananchi Viongozi wakiona.
 
Kitu cha Tatu; Kinacholigharimu Bunge letu kiasi cha kuingia kwenye vurugu, ni  laana ya kufunika makosa (Mithali 27:9) “Afunikaye kosa hutafuta kupendwa; Bali yeye akashifuye neno hutenga rafiki. Bunge na hasa Kiti cha Spika, kina Tabia ya kufunika makosa, kuzima hoja ambazo Mungu anataka wahusika waaibishwe.
 
Laana ya Tatu ni kuacha kutetea Walalahoi na Kukomesha Utekaji na Mauaji mbalimbali yanayotokea nchini, ambapo Damu ya Watu isiyo na hatia imekuwa ikimwagika bila huruma; (Mithali. 27:5) Amdhihakiye maskini humsuta Muumba wake; Naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu”.
 
Ya Nne na la Tano ni dhambi ya Rushwa kwenye Chaguzi  mbalimbali iliyopeleka baadhi ya wabunge Mjengoni hapo, sasa Mungu anakataa wahusika wasifanye Kazi yake maana mikono yao michafu. (Mithali 27:23) “Asiye haki hutoa rushwa kifuani, Ili kuzipotosha njia za hukumu.
 
Viongozi wengi wamesikiliza Uongo na Porojo za baadhi yao na kuziamini , hivyo kupotoa haki za wenye haki wakitumia Ndimi, Midomo na Masikio yaliyoumbwa na Mungu. Mithali 27:4 Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu; Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.
 
Heshima na Busara ya Mtu, Serikali, Taifa au Chombo chochote kinachoasisi Jamii, huwa yapo Kinywani, Ulimi na Maneno. Ukiona Kinywa, kinaridhia na kufinyanga maneno mabaya, na Ulimi ukaruhusu Maneno hayo yatoke, Nyongo ya busara imekufa.
 
Maandiko ya Kitabu cha Busara na Hekima (Mithali. 17:28) kinasema, “ Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu”.
 
Mithali. 17:12-13 inasema, Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang'anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wakeYeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake. Katika hili Mabaya hayataondoka bungeni hadi haki  ya kweli ya wananchi izinagatiwe. Je, Tusemeje Juu ya Bunge letu, Limelaaniwa?
 
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308 

4 comments:

  1. ulioanikwa hapo juu ya bunge; ni ukweli mtupu! hongerea sana mwandishi. kwa nini na wachambuzi kama hawa, hawatumiwi na vyombo vikubwa? big up kaka, unajua kuonya na kushauri

    ReplyDelete
  2. nasoma sana blog hii, huyu jamaa ni mwandishi na mchambuzi mzuri, mwajiri wake amuongeze mshahara, tunamuombea sisi wasomaji. je yupo dar sehemu gani? nina mambo nataka anisaidie kuandika. kipakacha ubungo

    ReplyDelete
  3. huyo bro alikuwa askari nini! maana haogopi kusema kweli na nimfuatiliaji wa bunge sana

    ReplyDelete
  4. .............tena habari zake nyingi ni za kuwasaidia wananchi wa vijijini..........mleteni da huyo......atafanya kazi nzuri sanaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Pages