Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Emmanuel Elibriki ‘Ney wa Mitego’ amesema asilimia kubwa ya wasanii
ambao wanashuka kimuziki ni wale ambao wanakua wameingia katika maswala ya
ndoa.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Ney alisema wasanii wengi wa bongo wanakurupuka katika hilo na
ikitokea ambaye amejipanga ni wachache sana na hapa bongo hajaona.
“Wasanii wengi wa bongo
tunakurupuka na hatujipangi katika mambo ya familia zetu na ndio maan aikitokea
msanii anaoa basi ujue lazima atashuka kimuziki,” alisema Ney.
Katika hatua nyingine, mkali
huyo alimpongeza msanii mwenzake, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ kwa kuwa na
mpango wa kuoa hivi karibuni.
“Diamond ni mdogo wangu, nampa
hongera kwa kutaka kuingia katika maisha ya ndoa hilo sio swala dogo namuombea
afanikishe mipango hiyo,” alisema.
Diamond ametangaza kwamba
anatarajia kufunga ndoa miezi miwili ijayo na kusema kwamba anaamini kwa
kufanyahivyo utakua ni hatua moja wapo ya kuzidi kufanikiwa kimaisha.
No comments:
Post a Comment