Na Mwanbdishi Wetu
KATIBU Mkuu Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Willigis Mbogoro, amesema mgogoro
wa Chama cha Ushirika Kagera (KCU), umekuwa ukichochewa kwa makusudi na
wanasiasa kwa ajili ya maslahi yao
binafsi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015.
Akizungumzana na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Mbogoro, alisema kutokana
na mkutano mkuu uliyofanyika hivi karibunu, kwa amani umemedhirisha kuwa chama
hicho hakina mgogoro, taarifa zinazosikika kuwa kuna mgogoro si za kweli.
Alisema TFC kama taasisi ya kulinda na kutetea haki na
maslahi ya vyama vya ushirika nchini, hawana nia ya kutetea utendaji kazi wa KCU
bali wanaomba wanasiasa nchini na wafanyabiashara kwa pamoja washirikiane na
chama hicho ili kuondoa changamoto zilizopo na kuboresha utoaji wa huduma kwa
wakulima wa kahawa katika mkoa wa Kagera, kwa kuwa hakuna mbadala wa ushirika
katika biashara ya kahawa katika mkoa huo, nchini kwa ujumla.
Mbogoro alisema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa na
wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitoa shutuma kwa chama hicho, ambazo
kulingana na sheria ya ushirika no. 20 ya 2003 hazina misingi kwani maamuzi
yote yamekuwa yakifanyika kupitia mikutano mikuu ambayo ndio yenye uamuzi wa
mwisho katika sheria ya ushirika.
“Hawa wanasiasa wamekuwa na nia ya kukigawa chama hiki
katika majimbo ili majimbo hayo waweze kuja kuyatumia katika uchaguzi mwaka
2015 vile vile wafanyabiashara nao nia yao
ni kuona migogoro inatokea kwemye vyama vya ushirika ili nao wapate nafasi ya
kuendesha bishara hizo”alisema.
Mbogoro alisema watu hao wamekuwa wakianzisha migogoro
katika maeneo mbalimbali ya nchi kama vile
migogoro inayoendelea kitokea kwenye mikoa ya Tabora, Mtwara, Mwanza Pwani na
kwingineko, kitendo ambacho kinaondoa ile nadharia ya uchumi ni kushirikiana.
Aliongeza kuwa ni wakati sasa kwa wanasiasa na
wafanyabiashara kushirikiana na KCU na si kubeza mafanikio ambayo yamepatikana ndani ya
miaka 60 tangu kuasisiwa kwake, na kukifanya kuwa chama pekee komgwe kuliko
vyote nchini.
Akizungumzia mafanikio ya KCU LTD katika kipindi cha miaka 50
iliyopita, Mbogoro, chama hicho ni taasisi ya kwanza kujenga shule za sekondari
ambazo ni Kisheju, Mugeza na Kashozi, shule hizo zinatoa elimu kwa watoto wa
Wanaushirika bure.
Alisema takwimu za miaka mitano iliyopita inaonesha mkulima
alilipwa si chini ya asilimia 80 ya bei ya soko la dunia ambako mwak jana KCU
ililipa zaidi wakulima ukilinganisha na bei ya soko la dunia kwa sh bilioni
2.5.
Mbogoro alisema mafanikio mengini ni kwa chama hicho
kudumisha amani, umoja na mshikamano kwa wakulima wa kahawa na wajasiriamali wa
mkoa wa huo wa Kagera.
No comments:
Post a Comment