Msanii machachari wa Bongo Flava, Barnaba, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Matembezi ya Hisani ya 'Step Ahead Walk 2013,' yatakayopambwa na kibao chake kiitwacho Wanawake alichoimba kwa ushirikiano na Mrundi anayefanyia shughuli za muziki nchini Kenya, Jean Pierre Nimbona 'Kidumu.'
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Barclays, Tunu Kavishe, akizungumza na waandishi wa habari (hawao pichani), wakati wa uzinduzi wa Matembezi ya Hisani ya Step Ahead Walk 2013 yatakayosindikizwa na Barnaba na Kidumu.
DAR ES SALAAM, Tanzania
'Step Ahead Walk’ ni mkakati endelevu wa Benki ya Barclays, ambao kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii. Matembezi hayo ya kila mwaka, yalizinduliwa mwaka 2008 hapa nchini na kusaidia kuelimisha jamii kuhusu uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto
KIBAO
cha ‘Wanawake,’ kilichoimbwa na nyota Bongo Flava Barnabas Elias, akishirikiana
na Mrundi Jean Pierre Nimbona ‘Kidumu,’ kimezinduliwa rasmi leo na kutangazwa
kupamba Matembezi ya Hisani ya ‘Step Ahead Walk 2013,’ yanayoratibiwa na Benki
ya Barclays Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Mahusiano wa Barclays, Tunu Kavishe, alisema maudhui ya wimbo huo ni kuhamasisha
wadau kujitokeza kwa wingi kushiriki ‘Step Ahead Walk’ ambayo lengo lake ni
kuchangisha pesa kwa ajili ya kinamama na watoto wachanga.
Aliongeza
kuwa, tukio hilo litafanyika Juni 8, 2013, katika hoteli ya Golden Tulip,
likihusisha matembezi ya hisani ya kilomita tano, ambapo kila mtu katika jamii
anakaribishwa kushiriki kwa kununua tiketi kwa silingi za Kitanzania 5,000 ambazo
zinapatika katika matawi ya Benki ya Barclays kuanzia Aprili 29.
“Mwaka
2011, Benki ya Barclays na washiriki wake walifanikiwa kukusanya shilingi mil.
150 kutokana na mauzo ya tiketi na matoleo mengine kutoka kwa wafadhili, lakini
mwaka huu lengo ni kuchangisha mara mbili ya kiasi hicho kutoka kwenye matoleo
ya washirika muhimu na washiriki wengine katika jamii,” alisema Kavishe.
Alibainisha
kuwa, kiasi kitakachochangishwa mwaka huu kitakwenda kusaidia katika masuala ya
uzazi na afya ya watoto, ikiwamo Mafunzo kwa wakunga wa uzazi, matibabu ya
Fistula na upasuaji kwa watoto waliozaliwa na ulemavu unaosababishwa na uzazi.
‘Step
Ahead Walk’ ni mkakati endelevu wa Benki ya Barclays, ambao kusudi lake ni
kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii. Matembezi hayo ya kila
mwaka, yalizinduliwa mwaka 2008 hapa nchini na kusaidia kuelimisha jamii kuhusu
uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto.
Kavishe
alisisitiza kuwa, ‘Step Ahead Walk 2013’ itafanikiwa, kama tu itawezeshwa na
kila mshiriki na jamii nzima ya Kitanzania, kwa hiyo akawataka wadau kujiunga katika
matembezi hayo ili kuweza kuleta mabadiliko katika masuala ya afya ya Uzazi na
Mtoto kwa ujumla hapa Tanzania.
Habari Mseto Blog
No comments:
Post a Comment