Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (pichani) amechaguliwa kwenye mchakato wa kumtafuta
“kinara wa Benki wa Afrika” kwa mwaka
2013 unaoendeshwa na African Banker
Awards chini ya African Development Bank
Group.
Kinara wa Benki wa mwaka ni tuzo inayotolewa kwa Viongozi (CEO`s) wa
sekta ya benki na fedha barani Afrika ambao wamepata mafanikio makubwa kwenye
mashirika yao hivyo kuleta maendeleo katika sekta fedha na uchumi katika nchi
zao na Afrika nzima kwa ujumla.
African
Banker Awards imechagua vinara watano wa
sekta ya fedha Afrika kuingia katika
mchakato huo ambapo mmoja wao ndiyo atakayejitwalia tuzo hiyo. Zaidi ya Dkt.
Charles Kimei, wengine waliongia kwenye mchakato huo na nchi wanazotoka kwenye
mabano ni Segun Agbaje-GTB Bank(Nigeria),
Aigboje Aig-Imoukhede-Access Bank(Nigeria), Andrew Allly-Africa Finance
Corporation(Nigeria) na Jao Figuerdo- Unico Bank.
Dkt.
Kimei ni mtanzania wa kwanza kuingizwa kwenye mchakato huu tangu kuanzishwa kwa
tuzo hiyo zaidi ya miaka kumi iliyopita, na ni mtanzania pekee kwenye
kinyang`anyiro hicho ambacho kimekuwa kikitawaliwa na mabenki kutoka nchini
Nigeria na Afrika ya Kusini. Hii ni fahari kubwa kwa taifa letu kwani Dkt. Charles
Kimei ni mtanzania anayeongoza benki kubwa ya Tanzania inayoendeshwa na
watanzania wenyewe.
Dkt.
Kimei, ambaye ni mchumi mwenye stashahada ya uzamivu, amefanya kazi katika
sekta ya fedha kwa zaidi ya miaka 30 akitokea Benki Kuu ya Tanzania alikokuwa
Mkurugenzi wa Sera na Utafiti kabla ya
kujiunga na Benki ya CRDB mwaka 1998 kama Mkurugenzi Mtendaji. Akiwa Benki ya
CRDB ameingoza kutoka Benki iliyokuwa ikijiendesha kwa hasara hadi kuwa Benki inayoongoza nchini.
Chini
ya uongozi wa Dkt. Kimei, Benki ya CRDB imeweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kutoka kutengeneza faida ya Shilingi
billion 2 mwaka 1998 mpaka kufikia Shilingi billion 108 mwaka huu, kuongeza
mtandao wake wa matawi kutoka matawi 16 hadi matawi 97 mwaka huu. Katika
kipindi hiki pia Benki ya CRDB imekuwa
kinara wa kuleta bidhaa bunifu kwenye soko ikiwemo kadi zenye nembo za
kimataifa za MasterCard na Visa, ATMs za kutolea na kuweka fedha, mashine
maalum za kulipa kwa kutumia kadi (POS), Mikopo maalum ya Microfinance na
Wajasiriamali pamoja na kushinda tuzo za kimataifa za Chapa Bora yaani
SuperBrands kwa miaka minne mfululizo (2010-2013) na tuzo ya benki bora itolewayo na Euro-Money mwaka 2004.
Chini
ya uongozi wa Dkt. Kimei, Benki ya CRDB imekuwa benki ya kwanza ya kizalendo kuvuka mipaka na kufungua kampuni tanzu katika
nchi jirani ya Burundi hivyo kufungua milango ya ukuaji wa mahusiano ya
biashara kati ya nchi hizo mbili na ukanda mzima wa Afrika Mashariki kwa
ujumla.
Kuingia
kwa Dkt.Kimei kwenye mchakato huu wa kupata kiongozi bora wa Benki wa Afrika kunakuja muda mfupi tu
baada ya kuteuliwa kwake bila kupingwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki
nchini Tanzania (TBA). Mwenyekiti wa Chama Cha Mabenki huchaguliwa na benki
zote wanachama wa TBA.
Tunamtakia
kila kheri Dkt.Charles Kimei na Benki ya CRDB katika kuipeperusha vyema bendera
ya Tanzania katika tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment