Mashabiki wa Wigan na Manchester City, wakiingia kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, kushuhudia mechi ya fainali ya Kombe la FA, iliyoisha kwa Wigan kuichapa Man City bao 1-0 na kutwaa ubingwa wa kwanza katika miaka 81 ya historia yake.
Huyu ni shabiki wa Man City akiwa mwenye furaha kabla ya kuanza kwa mechi hiyo. Mkono wake wa kushoto ameshikilia skafu ya timu yake na mfano wa kombe la FA.
Wigan haikuwa nyuma, huyu ni shabiki wake aliyejipaka rangi na kujiandika WAFC katika kichwa chake, ambayo ni kifupisho cha Wigan Athletic Football Club.
Wasanii wanaounda kundi maarufu la Royal Philharmonic Orchestra, wakiimba kibao chao kiitwacho Abide With Me, kabla ya kuanza kwa pambano la fainali ya Kombe la FA kati ya Wigan na Man City.
Mwali akitolewa na kuwekwa hadharani, dakika chaache kabla ya kuanza kwa pambano hilo.
Roberto Mancini akisalimiana na mmiliki wa Wigan, Dave Whelan.
Mmiliki wa Wigan, Dave Whelan akiingia uwanjani kushuhudia mtanange huo.
Wachezaji wa Wigan wakiomba dua kabla ya kuanza kwa pambano hilo la kukata na shoka lililomalizwa na bao la mtokea benchi Ben Watson dakika ya 90.
Carlos Tevez akipiga mpira adhabu mbele ya ukuta wa wachezaji wa Wigan.
Guu la mwanaume hilo; Hii ni miguu ya mshambuliaji Serigio Kun Aguero, likionesha aina mpya ya kiatu anachotumia katika siku karibuni.
Aguero akisikitika kupoteza moja ya nafasi muhimu za kuifungia timu yake katika pambano hilo.
Samir Nasri wa Man City akiwania mpira na beki wa Wigan
Mwamuzi akimuonesha beki Pablo Zabaleta wa Man City kadi ya pili ya njano.
Kocha wa Man City, Roberto Mancini, akiwa na msaidizi wake Brian Kidd wakifuatilia kinachojiri dimbani.
David Silva wa Man City, akipiga 'tik-tak' kujaribu kufunga.
Carlos Tevez akipiga kujaribu kufunga bila mafanikio.
Joe Hart akijaribu bila mafanikio kuzuia kichwa cha mtokea benchi Ben Watson kisitinge nyavuni.
Wachezaji wa Wigan wakishangilia bao hilo.
Roberto Martinez kushoto, akishika taji la FA na mmiliki wa Wigan Dave Whelan.
Martinez kulia akiwa na taji la ubingwa wa FA na mfungaji wa bao pekee, Ben Watson.
Wachezaji na maofisa wa Wigan wakishangilia kwa kumnyanyua juu kocha Martinez.
Wachezaji wa Wigan wakipiga picha ya pamoja na kombe lao la FA.
No comments:
Post a Comment