LONDON, England
Aidha, Toure anaamini kuwa kustaafu ghafla kwa kocha Sir
Alex Ferguson wa Manchester United, kutaingozea nguvu na kuibeba Man City
katika msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya ndani
MANCHESTER City leo inashuka kwenye Uwanja wa Wembley kuivaa
Wigan katika fainali ya Kombe la FA, huku kiungo wake Yaya Toure (pichani kulia), akitamba
kupania kuibebesha Man City ubingwa kama alivyofanya mwaka juzi.
Akizungumzia pambano hilo ambalo Man City inajiandaa
kuthibitisha ubora wake kwa kutwaa taji la tatu katika miaka mitatu, Toure
alisema alisaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo ili kuwa sehemu ya historia ya
klabu hiyo na nafasi hiyo ataitumia vema.
“Kila mwaka ni muhimu kwa klabu kwa sababu tunataka hii
kuifanya kuwa moja ya klabu kubwa.
Tumelitema taji la Ligi Kuu kwenda kwa
mahasimu wetu Man United, lakini sasa tutaka kutwaa ubingwa huu.
“Tunatakiwa lazima tutwae ubingwa, hiyo ndio sababu ya mimi
kusaini mkataba mpya. Nataka kuwa sehemu ya historia ya klabu hii.
“Tayari tumelianza hilo, kwa kuwa tumeshaanza kutwaa baadhi
ya mataji.
“Nina matumaini kwamba kuna mengine zaidi yanakuja hapa,
kama vile Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu na Kombe la FA,” aliongeza Toure.
Toure, 29, alikuwa shujaa wa Man City miaka miwili iliyopita
ndani ya Uwanja wa Wembley, ambako
alifunga mabao mawili moja katika nusu fainali dhidi ya Man United na jingine
kwenye fainali dhidi ya Stoke City.
Kiungo huyo alisema: “Hiyo ilikuwa moja ya fainali za aina
yake kwangu mimi. Nilifanya mashambulizi na kufunga na kwa sababu hiyo
nikapeleka medali ya ubingwa Etihad na kwa mashabiki kwa ujumla.
“Hilo lilikuwa jambo muhimu ambalo tulikuja hapa kwa ajili
ya kupata mafanikio,” alitamba Toure.
Aidha, Toure anaamini kuwa kustaafu ghafla kwa kocha Sir Alex
Ferguson wa Manchester United anayerithiwa na David Moyes, kutaingozea nguvu na
kuibeba Man City katika msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya ndani.
Man City ambao wamekuwa wapinzani wa karibu wa Man United
katika miaka miwili sasa ya ligi hiyo, wanahisi nguvu ya United itakuwa
imepungua kwa kuondoka Ferguson Old Trafford.
“Man United ni klabu kubwa na Ferguson ni mbobevu aliyeleta
mafanikio pale. Amejenga kila kitu ndani ya United na uwiano, ninatumaini, hamasa
itakwenda upande wa Man City kwa sasa.
“Tutaona msimu ujao. Kutakuwa na upinzani mkubwa kati ya Chelsea,
Liverpool, Arsenal na Man United. Tottenham nayo inakuja kwa kasi na ni wazi
kutakuwa na Ligi Kuu ngumu mno.”
The Sun
No comments:
Post a Comment