HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 22, 2013

VURUGU ZAENDELEA MTWARA, MMOJA ADHIBITISHWA KUFARIKI KATIKA VURUGU HIZO

 Gari la wagonjwa la Manispaa ya Masasi likiteketea kwa moto baada ya kutokea vurugu leo.
 Barabara ikiwa imefungwa kwa kuweke magogo na mawe.
 Mkazi wa Mtwara akinawa uso baada ya kupigwa mabomu ya machozi.
 Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria.
 Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria ya miguu.
 Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria..
 Magari ya Watumishi wa Umma yakiungua kwa moto.
Ofisi za Elimu Masasi.
Mitaa kadhaa ikiwa haipitiki baada ya kuchomwa matairi ya gari.

Mtwara, Tanzania


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 21 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara leo, zilizosababishwa na makundi ya vijana kuchoma moto, majengo ya ofisi za umma, nyumba za watu na kufunga barabara.

Hali hiyo imetokana na hotuba ya Waziri wa Nishati Prof. Sospeter Muhongo akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar wakati kauli mbiu ya Wananchi wa Mtwara ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni" 


Wananchi walalamikia kituo cha Television na Radio TBC kuzuia na kukata mawimbi yake kutoonekana wala kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa muda. 


Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam wakati Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara wakacharuka!


Kufuatia tukio hilo  Daraja la Mikindani limevunjwa na wananchi wenye hasira pamoja na kuchoma moto Jengo la Ofisi ya CCM saba saba. 




Nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia yachomwa moto.

Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwa ajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.


Kutokana  na hali hiyo watu walikimbia ovyo mitaani na watoto wamefungiwa mashuleni huku walimu walimu pia wakikimbia kutoka katika vituo vyao vya kazi. 


Katika maeneo ya Magomeni-Mtwara milio ya irsasi na mabomu ya machozi ndio ilikuwa imetawala na kusababisha hofu kubwa.


Kutokana na hali hiyo huduma zote za kijamii zimefungwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages