Logo ya klabu ya FC Vito iliyo chini ya Kituo cha Michezo cha Sports Development Aid (SDA), kilicho katika Manispaa ya Lindi.
Mkurugenzi wa SDA, Chigogolo Mohammed (wa kwanza kulia
nyuma), akiwa katika picha ya pamoja nje ya ofisi za kituo hicho na baadhi ya
wachezaji wa FC Vito. Kushoto nyuma ni Mratibu wa SDA, Ramson Lucas na Kocha
Jamal Lisuma.
Mkurugenzi wa SDA, Chigogolo Mohammed (wa kwanza kushoto
nyuma), akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha kwanza cha FC Vito. Kulia
nyuma ni Mratibu wa SDA, Ramson Lucas na katikati ni Kocha Jamal Lisuma.
Baadhi ya nyota wa FC Vito wakiwa katika meza ya chakula.
Mratibu wa SDA, Ramson Lucas akiwanoa yoso wa FC Vito alipokamata kwa muda jukumu la Kocha Jamal Lisuma ambaye ndiye kocha wa kikosi hiki.
Wazazi na walezi wa vijana wa timu ya FC Vito, wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji hao (waliovaa track-suit za bluu), katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika mjini Lindi hivi karibuni.
Juu: Wachezaji wa FC Vito wakimsikiliza mmoja wa wageni aliyetembelea mazoezi ya kikosi hicho na kupata nafasi ya kuzungumza nao.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Helsinki Cup ni
michuano ya wiki moja kila mwaka, ambapo mwaka huu itahusisha zaidi ya timu za
vijana 860 kutoka nchi 23 duniani, zitakazoumana katika soka la vijana wa kike
na kiume walio chini ya miaka 11
TIMU ya soka ya vijana ya FC Vito ya Lindi Mjini, kesho inatua
jijini Dar es Salaam, ikiwa safariki kuelekea Helsinki, Finland, inakokwenda
kushiriki Michuano ya Kombe la Helsinki, linalotarajia kuanza kutimua vumbi
Julai 8 na kumalizika Julai 13.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Mkurugenzi wa
Kituo cha Sports Development Aid (SDA), kinaichomiliki FC Vito, Mohammed
Chigogola, alisema kuwa kikosi chake kinatarajia kuwa Dar es Salaam kwa siku
mbili, kabla ya Jumatano kusafiri.
Aliongeza kuwa, wakiwa Dar, Jumanne wanatarajia kufanya
mkutano na vyombo vya habari utakaofanyika Ubalozi wa Finland nchini, ambapo watatumia nafasi hiyo
kuelezea mambo kadhaa yahusuyo safari yao
hiyo.
Kwa mujibu wa Chigogola, Helsinki Cup ni michuano ya wiki moja kila
mwaka, ambapo mwaka huu itahusisha zaidi ya timu za vijana 860 kutoka nchi 23
duniani, zitakazoumana katika soka la vijana wa kike na kiume walio chini ya
miaka 11.
Chigogola aliongeza kuwa, msafara wa FC Vito utakuwa na
jumla ya watu 15, wakiwamo viongozi watatu na wachezaji 12.
Aliwataja viongozi watakaosafiri na kikosi hicho pamoja nay
eye kuwa ni Mratibu, Ramson Lucas na Kocha Mkuu Jamal Lisuma.
Akiwataja nyota waliochaguliwa kuwamo katika msafara huo,
kocha Jamal Lisuma aliwataja kuwa ni Mohammed
Mussa, Osama Aman, Ramadhani Hassan, Abdul Mussa, Abdallah Mbade, Karim Bakiri,
Juma Msafiri na Ashrafu Hassan.
Wengine ni pamoja na Mohammed Selemani, Hossam Hassan,
Dominic William na nahodha Humphrey Lambaert. 10.
Katika mahojiano na Tanzania Daima, Kocha Jamal anaenda
mbali zaidi na kusema anajisikia furaha
kuwa kocha wa kikosi hicho, sio kutokana na kupata nafasi ya kusafiri,
bali kwa namna viongozi wa kituo wanavyompa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu
yake.
“Najivunia ushirikiano ninaopata katika kufanikisha program
zangu. Uongozi unanisikiliza na kunipa kila ninachohitaji katika kuwezesha
kikosi kuwa fiti kiakili, kimwili na kimbinu, hivyo kuwapa uwezo wa kupokea
vema mafundisho yangu,” anafafanua Jamal.
No comments:
Post a Comment