HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2013

BARNABA AJIPANGA KUACHIA ALBAMU YA TATU



Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnaba ‘Barnaba’, anajipanga kuachia albamu yake ya tatu itakayokuwa na nyimbo kumi, ikibebwa na jina la wimbo ‘Nimeona’.

Kwa mujibu wa Barnaba, albamu hiyo ataisambaza wiki hii kwani sasa yuko katika hatua za mwisho za kuikamilisha.

Alisema katika albamu hiyo kutakuwa na nyimbo nyingi ukiwemo ‘Sorry’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio, ikiwa ni mtililiko wa kuwapa burudani mashabiki wake.

“Hadi sasa hivi nina nyimbo saba ambazo ziko tayari na naendelea kuziandaa, naomba mashabiki wangu waipokee vizuri albamu hiyo ambayo naamini itakuwa gumzo mitaani kutokana na nyimbo zilizomo ndani yake.

Mbali ya albamu hiyo, Barnaba amekuwa akiwika na albamu zake kama ‘Kilicho Changu’ na ‘Njia Panda’ ambazo zilifanya vizuri na kumweka kwenye nafasi nzuri kisanii.

No comments:

Post a Comment

Pages