KUMEKUWEPO na wimbi la baadhi ya Mahakimu,
kutokuwepo mahakamani kuhukumu kesi walizopangiwa kwa mfululizo, hivyo kushindwa
kuhukumu kesi na kukwamisha mwendelezo wake na watuhumiwa kurudi bila kesi zao
kusikilizwa.
Hivi sasa wapo watu ambao wanateseka na
kukaa gerezani kwa muda mrefu kwa sababu tu, watendaji na Hakinu hawapo, ambapo
kukosekana kwao hakuoneshi mashiko zaidi ya kuwa na sababu nyepesi, na linalokwamisha
kesi husika zisiendelee mahakamani.
Mahakama zimekuwa kama zinawaadhibu watu
wasio na hatia! ambapo ningeitaka Mahakama na serikali kukomesha tatizo hilo na
kuacha kuwaadhibu watu bila sababu! Ikibidi Hakimu asipokuwepo, awekwe Mbadala
kazi iende.
Ningependa, ikitokea Hakimu hayupo, ni
vizuri Uongozi wa Mahakama uweke Mbadal wake, kuliko kuacha watu wasubiri hadi
wiki nyingine tena huku Watuhumiwa wakiendelea kukaa mahabusu bila sababu.
Sioni sababu za msingi zinazosababisha kesi
zisizohitaji uchunguzi ambazo uchunguzi wake umekamilika kutotolewa uamuzi
haraka, hasa wakati mwingine mtu kakanyaga Nyanya au hakuvaa Kofia Gumu (Helmet),
apewe Faini aende.
Ni rai yangu, Serikali na Wiziri ya Katiba
na Sheria na Ofisi hiyo, iweke muda maalum ambapo kesi za Jinai kwa mfano, Kesi
za Madai, Biashara na kadharika, ziwe na muda ambao Ukifika, lazima kesi hizo
ziwe zimekwisha.
Tukifanya hivyo tutawafanya mahakimu na
wanaowasaidia Polisi na Magereza, kuwajibika na kuisaidia Mahakama, kutimiza
malengo yao (Tentative Time), hivyo tunaweza kupima ufanisi wa vyombo hivyo na
kuvizawadia.
Ukifanye uchunguzi Magereza nyingi; Utakuta
Mahabusu wengi katika Magereza, hawafikishwi Mahakamani kwa sababu ya Mahakimu na
Watendaji wa Mahakama kutokuwepo kwa sababu ya Udhuru mbalimbali, na Mahakama
haiweki mbadala wake.
Kwa kuendekeza kuwaweka watuhumiwa kwa muda
mrefu, hasa kwa wale ambao Kesi zao ni za kudhulumiana au kuiba Njiwa, anakaa gerezani
kwa Gharama ya Bajeti ya Mahakama ya Wilaya au Mkoa, ni Matumizi mabaya ya
fedha.
Nafahamu kesi zikishafunguliwa mahakamani
sheria na kununi za uendeshaji zinataka kesi isikilizwe na itolewa uamuzi
mapema ila kama kuna sababu ya msingi inayosababisha kuchelewesha uamuzi.
Lakini si kesi ya kuiba Bata ikae miaka mitatu.
Tufike mahali Serikali, Bumge na Mahakama
kama vyombo muhimu (Mihimili Mitatu), watendaji wa Magereza na Polisi, waelewe
Thamani ya Kodi (Value for Money) ili tuwe na tahadhari ya Gharama hizo (Cost
Conscious).
Haingilii akilini kuwaweka wamachinga 100
gerezani, wakala Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya Robo mwaka, kwa kosa
la kutembeza Mitumba, kosa la kuvuka na nguo kulipokuwa na msafara wa Mgeni
toka nje. Huyu ni Mtanzania atembeze nguo wapi?
Wakati mwingine, kumekuwa na wingi wa kesi
zinazofunguliwa unaokinzana na idadi ndogo ya watumishi waliopo kwa sababu kesi
zingine ni ndogo zisizo na madhara kwa Taifa, mfano unamuweka ndani mzazi
ambaye hajalipa michango ya Shule ya Msingi! Aibu.
Mashahidi kusababisha kesi kuahirishwa mara kadhaa, mahabusu kutofikishwa
mahakamani, dharura kwa watendajii mahakamani, Hakimu, Mwendesha mashtaka, Wakili
wa utetezi, mshtakiwa na wazee wa baraza, haya yamo ni ya uwezo wetu.
Uhamisho wa mahakimu unaosababisha kesi zisiendelee hadi atakapopatikana
hakimu mwingine wa kuendelea kusikiliza kesi hiyo au kuanza upya kwa kadiri
sheria itakavyohitaji kwa kesi husika ambavyo naona ni kuviendekeza, maana
vinatatulika.
nyeregete@yahoo.co.uk 0757-933308
No comments:
Post a Comment