HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 21, 2013

Kala Jeremiah, Twanga Pepeta, Godzila, Jhiko Man kupagawisha ‘World Music Day’


Kala Jeramiah
Tamasha la muziki la kimataifa ambalo hufanyika Juni 21 kila mwaka la ‘World Music Day’ linafanyika leo Ijumaa katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo wanamuziki Kala Jeremiah, Ben Paul, bendi ya Twanga pepeta na wengineo wanaotamba katika tasnia ya muziki nchini watalipamba tamasha hilo.

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Umoja wa Ulaya wa taasisi za utamaduni (EUNIC) zikiwamo Aliance France-Dar es Salaam, Goethe Institut-Tanzania na British Council linalenga kutoa fursa kwa wanamuziki wakongwe na wachanga kukutana katika jukwaa hilo la kimataifa ambapo mashabiki wataingia bure.

Mratibu wa Tamasha hilo Abel Shuma ambaye pia ni Mratibu wa Shughuli za Utamaduni Alliance France Dar es Salaam, anawataja wanamuziki wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo kuwa ni pamoja na Godzila, Barnaba na bendi yake, mwanamuziki mkongwe wa Reggae Jhiko Man bila kusahau ngoma za asili kutoka kwa kundi la Super Maya Baikoko na Makini Kids.

Kala Jeremiah analielezea onyesho hilo kama mazao ya kazi nzuri aliyoifanya katika muziki wake “Nimepata faraja sana kualikwa kutumbuiza kwenye world music day, inaonyesha ni kwa jinsi gani muziki wangu unakubalika na kutambulika kitaifa na kimataifa".

Shirika la ndege la FasJet kupitia kwa Afisa Masoko Mtendaji Lucy Mbogoro linajivunia kudhamini tamasha hilo likitumia nafasi hiyo kurejesha shukran kwa Watanzania kwa mchango wao mkubwa katika shirika hilo kwa kuchagua kutumia huduma zake za usafiri wa anga.

Mbogoro anasema “World Music Day ni fursa nzuri ya kukutana na wadau wetu kwakuwa tamasha litawakutanisha watu wa mataifa mengi watapata kujua huduma zetu katika wakati huu tunaoelekea kuanzisha safari za ndege za kimataifa katika nchi za Afrika Kusini, Zambia na Rwanda”

Tamasha hilo ambalo limedhaminiwa na Fastjet, Pepsi, Total na balozi za Ujerumani na Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

Pages