HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

August 28, 2026

Mbeto ampongeza Ndejembi, alichopata Dkt. Nchimbi anastahiki

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

KATIBU wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Khamis Mbeto Khamis amempongeza Makamu wa Rais Mteule Deogratius Ndejembi na kubainisha kuwa kilichompata Dkt. Emmanuel Nchimbi kina mstahiki kutokana na kuonyesha dharau, jeuri na kiburi si kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) bali pia kwa Mwenyekiti wa chama ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake jana 28 Agosti 2026, CCM Kisiwandui mjini Unguja, Mbeto alisema kuwa  Kamati ya Usalama na Maadili CCM Taifa, chini ya Uenyekiti wa Mzee Steven Wassira ilimuta Dkt. Nchimbi Dodoma kwenda kutoa ufafanuzi au kuthibitisha kauli zake lakini bila sababu zozote za msingi hakutokea.



"Hakuwa nje ya nchi wala hakuwa na changamoto yoyote ya kumfanya asiende Dodoma" alisema Komredi Mbeto na kuongeza kuwa  Mwenyekiti kamati hiyo ambaye pia ni Makamu MwenyekIti CCM Taifa (Bara), Mzee Stevem Wassira ikaona kuna haja ya kumfuata Dar es Salaam.

Mwenezi huyo anabainisha kuwa Mwenyekit CCM Taifa, akawakodia ndege (ingawa sio utaratibu) wajumbe wa kamati hiyo ili kumfuata Dkt. Nchimbi Dar es Salaam ili wakutane nae sehemu waliyo ona inafaa ili athibitishe au kutoa ufafanuzi na tafsiri ya kauli zake, lakini hakutokea.

Komredi Mbeto alisema jitihada kubwa zimefanyika kumpa nafasi ili ajitetee lakini kwa masikitiko makubwa, hakuitumia na badala yake ameonyesha jeuri, dharau na kutoa visingizio visivyo na sababu na kukaidi wito huo.

Pamoja na yote CCM chini Mwenyekiti wake Dkt. Samia ambaye kutokana na kumuamini na kumpendekeza awe mgombea mwenza uchaguzi kuu uliopita, kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu Taifa, kilichofanyika 26 Julai 2026 Ikulu Ndogo Tunguu, akatumia uungwana akasisitiza aitwe kwenye Kamati Ndogo ya Maadili na Usalama ili asikilizwe katika kile ambacho kinaitwa tuhuma dhidi yake.

Komredi Mbeto alisisitiza kuwa alichopata kinamstahiki kwani hakuwa na nia njema na kauli zake na ameonyesha jeuri na dharau kubwa kwa chama na Rais Dkt. Samia ambaye ndie aliyempendekeza awe msaidizi wake.

Alisema Mbeto kuwa baada Halmashauri Kuu Taifa kupokea tuhuma dhidi ya Dkt. Emmanuel Nchimbi na yeye mwenyewe kushindwa kwenda kujitetea, ilijiridhisha pasipo shaka kuwa amepoteza sifa za uanachama wa CCM na uongozi.

Aidha kwa kauli moja Halmashauri Kuu CCM Taifa iliridhia kufukuzwa Dkt. Nchimbi uanachama na uongozo.

Pia ikaridhia kwa kauli moja jina la Deogratias Ndejembi lililopendekezwa na Mwenyekiti CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais.

"Hivyo hivi sasa linalofuata, ni jina hilo kupelekwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge kuwa Makamu wa Rais" alisema Komredi Mbeto.

Mwenezi huyo ambaye anasema CCM ni chama kikubwa kuliko mtu, anabainisha kuwa katika kikao hicho cha Tunguu mengi yaliibuka kumhusu na  mengine hata wajumbe wengine hawakuwa wanayafahamu.



"Adhabu ya usaliti CCM ni kufukuzwa uanachama kama ilivyotekelezwa kwa Dkt. Nchimbi" alisema Komredi Mbeto.

Dkt. Nchimbi kulingana na rekodi za CCM, mwaka 2016 alipewa onyo kali na Kamati ya Maadili na Usalama kutokana usaliti na kupinga maamuzi ya Kamati Kuu CCM Taifa mchakato wa kumpata mgombea Urais kupitia chama hicho 2015.

Komredi Mbeto anasema Makamu wa Rais huyo mteule anamfahamu toka wakiwa wajumbe wa NEC 2012 na anamtaja kama ni mchapakazi na amekuwa akionyesha ubora katika kila nafasi anayoteuliwa au kuchaguliwa" alisema.

Alitanabaisha kuwa uzinduzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP), hivi karibuni inaonyesha jinsi gani anavyojituma na kuwajibika.






No comments:

Post a Comment

Pages