Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiagana na Viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Luzaka Zambia kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia Mheshimiwa Hakainde Hichilema kufuatia ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia Uliofanyika tarehe 13 Agosti, 2026 ambapo Rais Hichilema alichaguliwa kwa Muhula mwengine wa Miaka mitano. Tarehe 01 Sept, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 01 Septemba, 2026, anaondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 13
Agosti, 2026, Rais Hichilema alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula
mwingine wa miaka mitano.
Ziara ya Rais Dkt. Samia inaendeleza uhusiano wa kindugu na
kihistoria kati ya Tanzania na Zambia, unaojengwa katika misingi ya umoja,
mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.





No comments:
Post a Comment