HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

August 23, 2026

MBETO: NAIBU ABDI ABAINISHA HAZINA YA VIONGOZI WAZALENDO ILIYOPO CCM

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAPOKEZI Makubwa aliyopata Naibu Katibu Mkuu (CCM) Zanzibar, Abdi Mahmoud Abdi Visiwan Pemba, hotuba zake kwa viongozi, wanachama wa chama chake na wananchi kwa ujumla vinayonyesha jinsi gani chama hicho kilivyo na hazina kubwa ya viongozi tofauti na vyama vingine vya siasa nchini.



Akizungumza na wanahabari Ofisi Kuu, CCM Kisiwandui kuhusiana na tathmini ya ziara ya Naibu Katibu Mkuu huyo, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi na Uenezi, Komredi Khamis Mbeto Khamis anasema chake kina hazina kubwa ya viongozi wenye uzalendo walio tayari kulitumikia Taifa lao.

Mwenezi huyo anasema, Mwenezi Abdi ambaye ni zao la Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) ambako pia amefanya mambo makubwa na ni hazina mojawapo ambayo anabainisha kuwa jina lake 29 Julai 2026, lilipowasilishwa katika Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu (CCM) Taifa, kilichofanyika Ikulu Ndogo Tunguu lilipitishwa na kuidhinishwa.


Komredi Mbeto anasema binafsi anamjua  Abdi kabla lakini utendaji wake akiwa UVCCM ndio uliofanya akaonwa Ofisi Kuu Kisiwandui, akalelewa na mtangulizi wake kwenye nafasi hiyo, Dkt. Mohammed Saidi Dimwa na hivi sasa anapomkabidhi mikoba chama kinamridhia kuitumikia nafasi hiyo akibainisha kuwa Rais Dkt. Mwinyi kaongezwa ‘jembe’ la kuwatumikia wananchi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, siku alipokwenda Ikulu kujitambulisha na kukabidhiwa majukumu, anasema hana shaka na utendaji wa Abdi.

“Nina ana imani na uwezo wake nikizingatia uzoefu na utendaji aliouonyesha akiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar akachape kazi kwa bidii kwa kushirikiana na viongozi na watendaji wa chama na kuendelea kuwatumikia wananchi kwa weledi na uadilifu” anaandika Rais Dkt. Mwinyi katika kurasa zake za jamii.

 


Naibu Abdi ambaye anasema kazi ya kwanza ni kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, anabainisha kuwa malipo yake kwa wanaCCM wenzake ni kufanya utumishi uliotuka kwa chama chao na kuhakikisha CCM inakuwa imara zaidi, inakuwa bora zaidi na inakuwa kimbilio la wanyonge na wananchi wa Zanzibar.



“Mimi na wenzangu tutafanyakazi kwa  kutumia katiba zetu, kanuni zetu na miongozo mbalimbali iliyopo katika chama chetu ili kukifanya CCM kiendelee kushika dola na jukumu hilo litalifanya kwa weledi mkubwa na kwa umadhubuti, umakini, utii mkubwa na kuhakikisha CCM kila chaguzi inayohusu dola, tunajipanga vizuri, tunajisimamia vizuri na hatimaye tunashinda vizuri.

Hayo yanatokea wakati Pemba ambayoi awali ilitajwa kuwa ngome ya upinzani hususan CUF wakati huo hadi ACT Wazalendo hivi sasa kugawanyika kutokana na kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo inayofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.


 

 



No comments:

Post a Comment

Pages