Na Mwandishi Wetu
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani, Mabere Marando,
amewaomba wakazi wa Kata ya Mianzini kumchagua Ngwata Saulo, ili akasimamie
fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Kata hiyo.
Marando alisema hayo wakati
alipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani
uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mbagara Rangi tatu wialayani
Temeke jijini Dar es Salaam.
Alisema mtakapo mchagua Saulo
mtakuwa hamkufanya kosa kwa kuwa Chadema inauhakika kuwa anao uwezo wa
kuchambua bajeti na kutambua ni kiasi gani cha fedha kimetengwa na Manispaa hiyo
kwa ajili ya maendeleo ya kata hiyo.
“Hata wasisi wetu wasiasa za
nchi hii, enzi hizo wakati walipokuwa wakiendesha siasa walikuwa na lengo la
kumng’oa mkoloni Mwiingereza hawakuwa wakipunzika kufanya siasa”alisema
Marando.
Alisema Chadema ni chama
makini cha upinzani chenye malengo ya kushika dola kwa kuking’oa chama tawala
madarakani, ndio maana hakipunziki kufanya kazi kwa ajili ya kuwakomboa
wanyonge kama Wanamianzini.
Marando alisema kutokana na
malengo hayo bado yanahitaji mshikamano wenu wa dhati kwa kumchagua mgombea wa
Chadema ambaye atakwenda kuwang’o mapanya wote wanaotafuna fedha zenu pale
Manispaa.
Naye mgombe udiwani wa chama
hicho Saulo, alisema atakapochaguliwa atahakikisha wenyeviti wa serikali za
mitaa wote wa kata hiyo, wanafutwa kazi kutokana na wenyeviti hao kushiriki
wenyevitendo mbalimbali vya kuwahujumu Wanamianzini.
“Mkinichagua nitamtaka
mkurugenzi wa wa Manispaa hii ya Temeke aitishe uchaguzi upya ili tuweze
kuchagua wenyeviti wapya ambao watafanyakazi kwa maslahi ya wanyonge bila
kubagua”alisema Saulo.
Saulo alisema atahakikisha
anapambana na wale wote waliojihusisha katika matumizi mabaya ya fedha za
miradi ya maendeleo akitolea mfano sh milioni 50 zilizotumika kujenga choo
kimoja chenye matundu kumi, bila kuonyesha kimejengewa wapi.
Naye Meneja wa Kampeni hizo
Jumaa Mwaipopo alisema Chama cha Mapinduzi (CCM), kimekuwaa kikishindwa katika
baadhi ya chaguzi kitendo ambacho sera zake hazikubaliki tena, ni wakati sasa
kwa wanamianzini kukiadhibu chama hicho kutokana na sera zake mbovu.
Uchaguzi huo mdogo unafanyika
katika kata hiyo baada ya kifo cha diwani Cecilia Macha (CCM), mwaka jana,
ambako uchaguzi huo utafanyika Juni 16 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment