Na
Mwandishi Wetu
MSHAURI wa ufundi
wa kamati ya maandalizi mbio za Tabora Marathon Tullo
Chambo, ameishukuru kampuni ya simu ya vodacom kwa msaada wa fulani 100
zilizotolewa jana jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwa niaba
ya wenzake alisema kuwa Vodacom imekuwa msaada mkubwa kwao kwa kuwezesha upatikanaji wa fulana hizo ambazo zitatumika
siku ya tukio juni 22.
“Tunaishukuru kampuni
ya mawasiliano ya simu ya vodacom ingawa
waliweza kutupatia fulana hizo kkwenye
hatua za mwisho lakini tunatambua mchango wao katika suala zima la michezo hapa nchini na tuna
omba waendelee na moyo huo”alisema Chambo
Akielezea maandalizi
ya mbio hizo zitakazofanyika mwishoni
mwa wiki hii,Chambo alisema kuwa hivi sasa wako kwenye hatua za mwisho ambapo
mbio hizo zitakuwa ni za kilometa 21 kwa wanaume,16 kwa wanawake pamoja na
kilometa 5 kwa watoto na watu wa umri wa kati.
Akikabidhi fulana hizo kwa niaba ya kampuni yake Matina Nkurlu
ambaye ni meneja mahusiano
alisema kwa kutambua umuhimu wa
michezo nchini ndiyo sababu kubwa iliyowasukuma kutoa udhamini wa fulana 100
kwaajili ya mashindano hayo .
“Vodacom Tanzania
itaendelea kudhamini na kuboresha
michezo hapa nchini ikiwa ni wadhamini wa ligi kuu Tanzania bara na pia jamii inapaswa kutambua kuwa kampuni
hii ni kwaajili ya watanzania”Alisema Nkurlu
Mbio za tabora marathon
zinatarajiwa kufanyika mkoani Tabora
Jumamosi ya juni 22 ambapo Vodacom
ni kati ya wadhamini wa mbio hizo
,Filbert Bay foundation ,NGF Company limited,
kampuni ya mabasi ya NBS,Emmanuel
Mwakaataka pamoja na Sarah
Ramadhani ambaye ni makamu mstaafu wa
Rais Chama cha riadha Nchini.
No comments:
Post a Comment