BARCELONA, Hispania
Chanzo cha ndani klabuni Nou Camp kimefichua kwamba, Rais
wa Barca amesisitiza kuwa klabu yake haitomuuza kiungo wake Fabregas, hata kama
Man United itatuma ofa ya tatu - baada ya mbili za awali kukataliwa
WAKATI klabu ya FC Barcelona ikiisisitizia Manchester United
kwamba kiungo wake mahiri Cesc Fabregas hauzwi, beki wa kati wa Barca, Gerard
Pique ameitaka klabu yake hiyo ya zamani kutopoteza muda kupeleka ofa ya tatu,
baada ya mbili kukataliwa.
Man United ilithibitisha juzi Jumatatu kuwania saini ya kiungo
na ikaboresha ofa yake na kufikia dau la pauni milioni 30, lakini taarifa
nchini hapa zikaeleza namna miamba hiyo ya Nou Camp ilivyokataa ofa hiyo.
"Fabregas hauzwi," chanzo cha ndani klabuni Barcelona
kilipasha Jumatatu jioni na kuongeza: "Rais wa klabu (Sandro Rosell),
ameweka wazi kila kitu kuhusu hilo kwa Man United."
Bosi mpya Old Trafford, David Moyes mapema hiyo hiyo juzi
alikiri kuwa uenda klabu yake ikalazimika kukubali kushindwa kwa jaribio lao
hilo.
Alipoulizwa kama anaweza kukata tamaa kumng’oa Fabregas Nou
Camp, Moyes alisema: "Nadhani hatua hiyo inaweza kuja, lakini nadhani
wakati unapoonesha nia ya kupata saini ya mchezaji mzuri, unatakiwa kutumia
kila nafasi, nami nitafanya hivyo.
"Mimi nina matarajio kwamba nitaendelea kupigania ujio
wake.
"Kwa sasa naweza kukwambia kitu kimoja kwamba, Ed
Woodward (Kaimu Mtendaji Mkuu Man United) anashughulikia hilo ili kuwezesha
utimilifu wake na tuna matumaini makubwa kuwa kila kitu kitakuwa sawa karibuni."
Aidha, Pique ambaye aliihama Man United na kutua Barca,
ameibuka na kuambia Red Devils kuwa: “Man United inapoteza muda wake.
“Ikumbukwe ilichukua muda mrefu kwa Fabregas kutimiza ndoto
yake ya kurejea nyumbani na kamwe hawezi sasa kuipoteza.
“Hapa ni nyumbani, ni sehemu ambapo familia yake ilipo, nay
eye akiwa hapa anacheza pamoja na marafiki zake wa karibu. Yeye ametuambia sisi
kuwa anajisikia furaha na fahari na angependa kuendelea kubaki nasi Nou Camp.”
BBC Sports/The Sun
No comments:
Post a Comment