HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2013

Mikataba ya Obama isiwe Siri, kama kuja kwake haikuwa siri

Rais Barack Obama wa Marekani akizungumza na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Na Bryceson Mathias
KWA muda mrefu nchi yetu imekuwa na tatizo la kusaini mikataba na wawekezaji na kuifanya kitu cha siri! Siri kwa Wabunge, siri kwa Viongozi na Siri kwa Wananchi wenye Rasilimali.
Ziara ya Rais Barack Obama toka Taifa kubwa kiuchumi, ni fursa muafaka kwa watawala wa Afrika na hasa Tanzania, na kujiona kama Mwanamwali wa Kizazi cha Ki-Maskini, aliyefanikiwa kuposwa na Mwana wa Mfalme, hivyo asiwe limbukeni.
Nasema hivyo kwa sababu, ikifika mahali Taifa pekee katika mengi lililotembelewa na Kiongozi wa Dunia kama Obama likipewa Misaada, halafu mikaaba yake ikawa Siri kama hapo awali, tutapata aibu na tutakuwa kama mtu anayeficha Msiba wakati Kilio kitamuumbua!.
Ujio wa Obama Tanzania unafananishwa na Esta katika Biblia, binti aliyekuwa hana baba wala mama. msichana huyu alikuwa wa umbo, mzuri na uso mwema; ambapo walipokufa baba na mama yake, Mordekai alimtwaa kuwa binti yake, kama Tanzania inavyotwaliwa na Obama (Esta 2:9-18), baada ya kuachwa na Nyerere, imeipendeza USA.
Basi ikawa, wakati iliposikiwa amri ya mfalme na mbiu yake, wasichana wengi wakakusanyika huko Shushani ngomeni mikononi mwa Hegai; Esta naye (Tanzania) aliingizwa katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake.
Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; naye akampa upesi vifaa vya utakaso, pamoja na posho zake, na vijakazi saba walio haki yake, wa nyumbani mwa mfalme. Pia akamhamisha na vijakazi wake akawaweka mahali pazuri katika nyumba ya wanawake.
Walakini Esta hakudhihirisha kabila yake wala jamaa yake, kwa maana ndivyo alivyomwagiza Mordekai asiwadhihirishe. Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kumiliki kwake.
Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya malkia badala ya Vashti.
Kama Rasilimali nzuri ya watanzania na kujibodoa kwao kwa maadili mema na Ustawi wake umeifikisha Marekani kupitia kwa Obama kuipa fursaTanzania kuwa Malkia wa kutembelewa kati ya nchi 54 za Afrika na kuwa Malkia Vashti achukue nafasi  yake, si wakati wa kufichana Mikataba iliyoingiwa ikawa ya Siri kwa wachache.
Jambo limgine ambalo nataka wanasiasa Uchwara wa Tanzania wajifunze kwa Obama, ni Jinsi ambavyo katika mazungumzo yake yote, hakudiriki kamwe kuzungumzia U-Democrats na U-Republicans wa nchini Marekani tofauti na fedhaha ya yetu.
Kubwa alizungumzia Utaifa, Uzalendo wa Marekani, isitoshe kama Rais wa Taifa kubwa na anayewakilisha wananchi wa Marekani, alionesha kupevuka na kukomaa kisiasa, hakuonekana kuwa na uchokozi na vijembe au kejeli za kiitikadi mwanzo wa hotuba hadi mwisho.  
Wako wana siasa wasio na upeo watajisahau na kuanza kujigamba na kujisahau wakidhani Itikadi ya chama chao ndio imefanikisha ujio wa Obama na kuvibetua Vyama vingine la hasha! Ni muhimu waelewe kilichomleta Obama ni Uzuri, Mwanamwali Tanzani.
Aidha Uzuri huo ni Fahari ya Rasilimali zake, Uchum na Utajiri ilionao usio wa Itikadi yoyote ya Chama fulani ila watanzania,  kama ambavyo mwenyewe amesema Nia yake ya kutembelea nchi yetu ni, Kiuchumi, Kibiashara, Kiafya na Kidemokrasia ambayo nchi inaelekea kuoza.
 nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308

No comments:

Post a Comment

Pages