Na Bryceson Mathias, Gairo
WANACHAMA na Wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Gairo, wamekanusha taarifa kuwa Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Omary Awadhi, alimwagiwa Tindikali usoni, isipokuwa wamedai aliandaa mbinu hiyo ili asihudhurie kikao cha kumng’oa madarakani 6.7.13.
Juni 29, mwaka huu katika mitandao ya Kijamii, kulikuwa na taarifa zilizosema Mwenyekiti Awadhi, alikuwa amemwagiwa tindikali usoni usiku nyumbani kwake Gairo na Magaidi wasiojulikana na kukimbizwa Dar es Salaam kwa matatibabu zaidi!.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ilidaiwa Mwenyekiti huyo alitokewa na tukio hilo usiku wa manane baada ya watu wasiojulikana kumgongea na kumwamsha, na Ghafla alipofungua Dirisha alihisi kumwagiwa kitu usoni kilichomletea maumivu makali na uso wake kuharibika.
“Kuna madai kumekuwepo na mvutano wa muda mrefu baina ya Mwenyekiti huyo na Mbunge wa Jimbo hilo la Gairo, Ahmed Shabiby, ulioshika kasi baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Abdalahamani Kinana hivi karibuni”.ilisema taarifa hiyo kwenye mitandao.
Katika ziara ya Kinana, ilidaiwa Awadhi alimtuhumu Mbunge huyo kukigawa CCM, yeye alipotangaza kugombea ubunge 2015, ambapo Kikao kilichosababisha mtafaruku huo ni cha Julai 7, 2013 kuhusu wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya, waliokusudia kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Mwenyekiti huyo.
Mbali ya madai, Magaidi waliokusudia kumdhuru walimtaka ajiuzuru na asihudhurie kikao hicho, jambo ambalo Awadhi alilipinga na kudai lazima atakihudhuria, na kudhaniwa ndicho kilichomsababishia amwagiwe Tindikali, akidai haikumdhuru sana baada ya kufunga Dirisha haraka na kunawa maji, jambo linalopingwa kuwa ni Muongo, wengi wakidai ang'olewe CCM.
Aidha Mbali ya Taarifa toka kwa mjumbe mmoja wa Jumuiya ya Wazazi (Jina linahifadhiwa) kudai mvutano wa muda mrefu baina ya wanasiasa hao, unakitkisa CCM Gairo, wanadai huenda Mwenyekiti huyo alitumia Ujanja huo ili asihudhurie kikao hicho Juni 6, 2013 ili asing’olewe katika kiti chake na wajumbe hao.
No comments:
Post a Comment