HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 21, 2013

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA SIKU MOJA WA TROIKA YA SADC JIJINI PRETORIA, AFRIKA KUSINI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijibu maswali toka kwa wanahabari wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini,  Jumamosi usiku. Kutoka kulia ni Rais wa Afrika Kusini Mhe Jacob Zuma, Rais wa Msumbiji ambaye pia ni mwenyekiti wa SADC Mhe  Armando Guebuza, Katibu Mtendajji wa SADC Dkt  Tomaz Augusto Salomão na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah.  (Picha na Ikulu)
  Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini,  Jumamosi usiku.
 Mwenyekiti wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Armando Guebuza baada ya mkutano wa kamati ya Troika  katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini,  Jumamosi usiku.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation). Kutoka kulia ni Mwenyeiti wa Chama cha Wataalam Watanzania waishio Afrika Kusini, Dkt Hamza Mokiwa, Mwenyekiti wa Tanzania Women in Gauteng (TWIGA), Mama Scholastica Kimario, Rais Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe Radhia Msuya, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Afrika ya Kusini Bw. Deusdedit Rugaiganisa na Bw. David Mataluma, mratibu wa Vijana katika Jumuiya ya Watanzania.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka  leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)

No comments:

Post a Comment

Pages