HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2013

TWIGA BANCORP KUTUIMIA MAWAKALA KUTOA HUDUMA ZAKE




Ofisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp Limited, Hussein Mbululo, akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na huduma mbalimbali za kibenki zinazopatikana katika katika Banda la Benki hiyo lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo (kulia) akizungumza na Wafanyakazi wa Benki hiyo waliopo Viwanja vya Maonesho sabasaba, Ofisa Masoko, Adebert Archerd  na Katikati ni Ofisa Uendeshaji wa shughuli za Kibeki wa Twiga Bancorp, Upendo Tendewa

 Wakazi wa Dar es Salaam wakiingia katika Banda la Karume lililopo jirani nja Banda la Twiga Bancorp.


 Mteja akipata huduma ya kuchukua Fedha katika mashine ya kutolea fedha ya Umoja Switch, hivyo wateja hawana haja ya kutembea na Fedha katika maonesho hayo.
 Wateja wakipata huduma na ushauri ndani ya banda hilo.
 Ofisa Uendeshaji wa shughuli za Kibeki wa Twiga Bancorp, Upendo Tendewa, akihudumia wateja walio fika katika banda la Twiga Bancorp kufanya shughuli za Kibenki.
 ********
BENKI YA Twiga Bancorp kuanzia mwezi oktoba mwaka huu inaanza kutumia mawakala   nchini ili kutoa huduma za kibenki kwa nia ya kupanua huduma zao kwa wananchi na kuongeza idadi ya watumiaji huduma za kibenki.

Kutokana na utumiaji wa mawakala kuanzia juzi  benki hiyo imebadili taratibu zake za kibenki na wanaendelea na kupanga taratibu kufikia leo hilo.

Mkurugenzi Mtendaji mkuu wa benki hiyo,Hussein Mbululo alisema hayo jana katika badna la maonesho lililopo viwanja vya sabasaba katika maonesho ya 37 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea .

Alisema katika kuanzisha utaratibu huo wa kuwa na mawakala  hao watawapatia vifaa katika kufanya huduma hizo za utaratibu wa kibenki huku wakihakikisha wakala ana duka lililopo maeneo yenye usalama.

“awali tulikuwa na mkakati wa kufungua kila mwaka tawi moja katika mikoa tofauti pamoja na kutumia vicoba lakini sasa tunapanua wigo kwa kutumia mawakala mbalimbali ifikapo mwezi huo”Alisema
Alisisitiza kuwa mwaka huu wamefungua tawi mkoani Dodoma huku wakitoa huduma ya kila wiki kwa vicoba katika wilaya ya Bunda

AKizungumzia maonesho hayo alisema wao wanashiriki kwa kuelezea huduma zao pamoja na kutoa huduma zote za kibenki huku wanaotumia huduma ya ATM za umoja wakipata huduma katika ATM zao.

Ili kukabiliana na wizi wa mitandao ,Mkurugenzi huyo alisema wamegundua kuwa kadi zao zilikuwa hazina ubora wa kutosha hivyo kutoa mwanya wa kufanyika kwa wizi hivyo wameamua kubadilisha kadi na kutengeneza zenye ubora zaidi.

Alisema benki hiyo iliishaibiwa kwa wizi wa mitandao zaidi ya sh.milioni 30  na kufanikiwa baadhi ya wezi hao kuwapata na sasa wamedhibiti mianya yote ya wizi.

“baada ya kuibiwa tulibaini kuwa kadi zetu zilikuwa na ubora wa chini hivyo tumezibadili na kuhakikisha muda wote benki zatu zinakuwa na ulinzi wa kutosha “Alisema .

No comments:

Post a Comment

Pages