Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania wakiwa katika kikao cha kwanza tangu bodi hiyo kuteuliwa ambapo kilijadili mambo mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji nchini. (Picha na Francis Dande)
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Salum Shamte akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza.
Mwenyekiti
mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya maazimio ya bodi hiyo kuhusu sera ya uwekezaji nchini. Kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa kikao cha kwanza tangu bodi hiyo iteuliwe. Kushoto ni mjumbe wa Bodi hiyo, Arnold Kileo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imetakiwa kusitisha mara moja mpango wake wa ugawaji
wa leseni za vitalu vya gesi hadi hapo itakapopatikana sera ya gesi ili kuwapa
fursa watanzania kumiliki vitalu hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti mpya wa
Bodi ya Taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi, alisema kuwa
endapo ugawaji wa vitalu hivyo utafanyika Oktoba mwaka huu kama ilivyopangwa,
watanzania hawatakuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali hiyo.
Dk. Mengi ambaye alikuwa akizungumzia maazimio ya bodi hiyo
iliyokutana mara ya kwanza jana tangu ilipoteuliwa hivi karibuni, alisema wakati
Serikali iko mbioni kufanya mnada wa vitalu hivyo saba vya gesi, hakuna
kipengere kinachomwezesha mtanzania kumiliki gesi hiyo.
Akizungumzia sera za uwekezaji kwa ujumla, Dk. Mengi alisema
taasisi hiyo inaitaka Serikali kuingiza kwenye Katiba mpya inayokuja kipengere
kinachowapa haki watanzania kuwa na ubia na wawekezaji wa nje badala ya
kuwaachia wageni hao kumiliki rasilimali za hapa nchini kwa asilimia 100.
Alisema hali hiyo itawawezesha watanzania kuwa na hali ya
kumiliki na kulinda rasilimali zao ambazo kwa sasa zinawanufaisha zaidi wageni
kuliko watanzania wenyewe.
“Sisi tunaitaka Serikali ihakikishe kuwa shughuli yoyote ya
uwekezaji wa kiuchimi, iwe na mtanzania ndani yake na watanzania hawa,
wasishindwanishwe na wawekezaji wakubwa wan je,” alisema Dk. Mengi.
Naye Makamu mwenyekiti Salum Shamte, alisema kuwa Serikali
inapaswa kuhakikisha sheria ya manunuzi za umma inawanufaisha zaidi watanzania
kuliko wawekezaji.
Alisema hivi sasa kiasi kikubwa cha fedha za Bajeti ya kila
mwaka, zinatumika katika kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma na kazi hiyo
imekuwa ikifanywa na wawekezaji badala ya kuwawezesha watanzania.
Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Dk. Mengi alisema kuwa asilimia
80 ya Bajeti ya mwaka huu wa fedha, itatumika kwa ajili ya manunuzi ya umma
hivyo ni vyema kazi hiyo ikafanywa na watanzania.
“Ukiangalia bajeti ya mwaka huu, karibu asilimia 80, sawa na
sh trilioni 14 zitatumika kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa na huduma za umma.
Fedha hizi zikiingia kwa watanzania, zitachangia sana kukuza uchumi wa taifa,”
alisema Dk. Mengi.
No comments:
Post a Comment