HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 18, 2013

KLABU ZA EPL, FDL DAR ES SALAAM ZAPIGWA MSASA

 Mgeni Rasmi wa Semina Elekezi ya Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu, akifungua semina hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa na kushirikisha klabu nne Ligi Kuu na saba za Ligi Daraja la Kwanza za mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo.
 Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto, akifuatilia kwa umakini semina elekezi ya DRFA. Wanaofuata baada ya Cannavaro ni Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, Kocha wa Makipa Yanga Razak Siwa na Katibu Mkuu wa Ashanti United, Aboubakar Silas.
 Ofisa Habari wa klabu ya Friends Rangers, Asha Kigundula (katikati), akisikiliza kwa makini mada mbalimbali katika semina hiyo ya DRFA.

DAR ES SALAAM, Tanzania

Katika semina hiyo, waashiriki walipata nafasi ya kuelimishwa na kukumbushwa juu ya majukumu yao kwa mada tatu za Sheria ya Mchezo iliyowasilishwa na Mkufunzi Omar Abdulkadir, Utoaji wa Habari iliyowasilishwa na Boniface Wambura na Masuala ya Ufundi iliyotolewa na Sunday Kayuni

CHAMA cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), jana kiliendesha Semina Elekezi ya siku moja kwa viongozi na manahodha wa Klabu za Ligi Kuu (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) za mkoa huo, tayari kwa changamoto ya msimu mpya wa ligi hizo.

Semina hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini, ambapo viongozi wa klabu 11 za madaraja hayo mkoa wa Dar es Salaam, zikiwamo nne za Ligi Kuu za Yanga, Simba, Azam FC na Ashanti United walihudhuria, pamoja na viongozi timu saba za FDL.

Viongozi, makocha na manahodha wa klabu za FDL waliohudhuria semina hiyo maalum kwa ajili ya kuwaongezea weledi wa kiutendaji kwa ustawi wa timu zao ni wa vikosi vya; Transit Camp, Green Worriors, Tesema, African Lyon, Villa Squad, Friends Rangers na Police Central.

Akifungua semina hiyo, Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, aliipongeza DRFA kwa harakati chanya za kunyanyua soka la klaabu za madaraja tofauti ya mkoa huo, huku akiitaka kusaidia timu za FDL kupanda Ligi Kuu na kuongeza idadi kutoka nne za sasa.

“Ili kuzipunguzia mzigo klabu zenu, mnapaswa kusaidia harakati za kuwa na timu nyingi za Dar es Salaam katika VPL, ambapo timu zitapunguziwa safari nje ya mkoa, ambazo ugharimu kiasi kikubwa cha pesa,” alisisitiza Zungu.

Akijibu agizo hilo, Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo, aliahidi upiganaji katika kufanikisha ushiriki mwema wa timu za FDL ili kupanda daraja, huku akiongeza kuwa, bado haoni timu ya kumudu kuuondoa ubingwa wa Ligi Kuu miongoni mwa timu za Dar.


Katika semina hiyo, waashiriki walipata nafasi ya kuelimishwa na kukumbushwa juu ya majukumu yao kwa mada tatu za Sheria ya Mchezo (iliyowasilishwa na Mkufunzi Omar Abdulkadir), Utoaji wa Habari (Boniface Wambura) na Masuala ya Ufundi (Sunday Kayuni).

No comments:

Post a Comment

Pages