Mwandishi Wetu, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi ( CCM) kimesema wakati ifikapo 05 Februari 2026 kikitimiza miaka 49 toka kuzaliwa kwake 1977, kinajivunia juhudi za kufikia shabaha na malengo ya kuundwa kwake.
Chama hicho kinasisitiza kuendelea kusimamia misingi ya Sera zake kwa kuendelea kuhubiri tija na faida ya ustawi wa amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis anaeza misingi ya chama hicho leo 04 Februari 2026, akiwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
Mbeto anasema kwa Miaka 49 Serikali za CCM zimemfanya mTanzania atoke katika kadhia ya unyonge wa kunyonywa, kunyanyaswa na kudharauliwa hadi kuwa mtu huru anayeheshimika.
CCM katika kuamini Umoja wa Afrika (AU), anasema Mbeto, kimeshiriki kikamilifu katika harakati zilizoleta Ukombozi wa Mataifa karibu yote yaliyopo, Kusini mwa Afrika.
Miaka 49 ya Sera za CCM, mTanzania amewekwa mbali Mtanzania amewekwa mbali na maadui Ujinga, Umasikini na Maradhi.
"Tunaelewa maadui hao ni kazi kumalizika kwa pamoja, mapambano dhidi yao yataendelea" anasema Mbeto.
Anabainisha kuwa, umadhubuti wa CCM utabaki katika kuziunganisha jamii, kufuta aina zote za unyonyaji, maonevu au jaribio lolote la kudhoofisha uchumi na kuzorotesha maendeleo.
"Kuwepo kwa vituo vya afya, zahanati na hospitali ni kumkabili adui maradhi. Kujenga Shule za Msingi na Vyuo Vikuu ni mkakati wa kufuta Ujinga.
Anasema Mwenezi Mbeto, miradi ya kilimo, uvuvi, ufugaji, ujenzi wa viwanda, barabara na masoko ni kumfanya kila mtu ajijenge kiuchumi.
Kuhusiana na ustawi wa maendeleo ya demokrasia ndani ya CCM, anasema ushiriki wa wanachama katika kuamua, kuchagua na kuchaguliwa ni kielelezo cha kukomaa kwa tasisisi hiyo.
'Kwa miaka 49 tumejenga taasisi imara, makini inayoaminiwa na kutegemewa na Wananchi wote. Pia sera na miongozo ya chama chetu imekuwa ikibadilka kulingana na mahitaji ya nyakati" anasema Mwenezi Mbeto ambaye chama chake hicho ndio kimekuwa kikiisimamia serikali katika kutekeleza Ilani na Sera za CCM kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.



No comments:
Post a Comment