Na
Elizabeth John
MKALI
wa muziki wa kizazi kipya, Sunday Mangu ‘Linex’, anatarajiwa kusambaza video ya
ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kimugina’ hivi karibuni.
Linex kwa sasa anatamba na kazi yake ya ‘Mahakama ya
Mapenzi’ mbali na kuwa na nyingine nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya
vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Linex alisema video hiyo anatarajia kuanza kuisambaza hivi karibuni
katika vituo mbalimbali vya televisheni na kwamba, tayari upo katika hatua za
mwisho kukamilika.
Alisema wimbo huo ni miongoni mwa vibao vyake ambavyo
ameviandaa kwa ajili ya mashabiki wake, hivyo wakae mkao wa kula kuipokea kazi
hiyo.
“Kila wimbo ninaoutoa lazima kunakuwa na kisa cha kweli
nyuma yake, hivyo kuna baadhi ya maneno yaliyoko humo ni ya kweli na mengine ni
stori tu, ambazo nimeamua kuwapa mashabiki wangu,” alisema Linex.
No comments:
Post a Comment