Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary
Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ anajiapanga kuachia albamu yake ya kwanza ambayo bado
hajaipatia jina kutokana na ubora wa nyimbo ambazo zipo ndani yake.
Dimpoz kwasasa anatamba na kazi yake inayokwenda
kwa jina la ‘Tupogo’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio,
ambayo amemshikisha mkali kutoka Nigeria, J. Martins.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa
msanii huyo, Mbarouk Issa
‘Mubenga’ alisema msanii huyo yupo
katika maandalizi ya albamu hiyo ambayo itakua na nyimbo kadhaa ambazo
zimefanya vizuri katika soko hilo.
“Kwasasa yupo katika maandalizi ya albamu hiyo, naomba
wapenzi wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hii ambayo naamni itakua na
birudani iliyokamilika kutokan ana mashairi ya nyimbo hizo kusimama,” alisema.
Mbali na ‘Tupogo’, msanii huyo alishawahi kutamba na kazi
yake za ‘Nai nai’, ‘Baadae’, ‘Me and You’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha
na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
No comments:
Post a Comment