BAADA ya kutamba na nyimbo mbalimbali katika muziki wa
kizazi kipya nchini, William Ngowi ‘Mabeste’ yupo mbioni kuachia kibao chake
kipya kinachojulikana kwa jina la ‘Nishauri’ ambacho amemshirikisha mkali wa
muziki huo, Peter Msechu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mabeste alisema, ngoma hiyo ipo tayari na kinachosubiriwa kumalizika kwa
sikuku za Idd ili aweze kuisambaza kwenye vituo mbalimbali vya radio.
“Mungu akisaidia, naweza kuachia pamoja na video,
lakini endapo hali haitokwenda sawa, nitaachia ‘audio’ halafu video itafuata
baadaye,” alisema Mabeste.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao kinachojulikana
kama, ‘Baadaye Sana’ kilichotengenezwa chini ya mtayarishaji Pancho, ambacho
kinafanya vizuri katika muziki huo.
Licha ya kutaka kuachia kibao hicho, Mabeste alishawahi
tamba na vibao kama ‘Dhahabu’ alichomshirikisha Dully Sykes, Chiku, Mr. Blue na
Mwana FA, ‘Pesa iko wapi’ pamoja na ‘Nacheza rafu’ ambazo ziliweza kufanya
vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini.
No comments:
Post a Comment